Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-MAREKANi-USALAMA

Jeshi la Israel laendelea kukabiliana na vurugu kufuatia tangazo la Marekani juu ya Israel

Maandamano kadhaa yalishuhudiwa siku ya Jumatano, Desemba 13, katika maeneo ya Palestina kulaani uamuzi wa Marekani unaotambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.

Vurugu zaendelea kushuhudiwa katika eneo la Beit El, katika Ukingo wa Magharibi, kufuatia hatua ya Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel..
Vurugu zaendelea kushuhudiwa katika eneo la Beit El, katika Ukingo wa Magharibi, kufuatia hatua ya Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.. REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Maandamano mengi yaligubikwa na machafuko yaliyosababishwa na makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya Israel, katika miji ya Hebron na Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi.

Makabiliano haya ya kila siku yanadumui wiki moja na majeshi ya Israeli yameamua kukabiliana na machafuko hayo.

Watu kadhaa walikamatwa katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na mmoja wa waanzilishi wa chama cha Hamas.

Jeshi la Israel limesema mashambulizi yake roketi yanazilenga ngome tatu za kijeshi za wapiganaji wa kundi la Hamas, ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi dhidi yao la kutoka ukanda wa Gaza.

Israel pia imeamuru kufungwa kwa mpaka kati yake na Gaza, baada ya shambulizi la nne la maroketi yanayodaiwa kurushwa na kundi la Hamas.

Hali hii ya mapigano ya kundi la Hamas inadaiwa kuwa ni kutokana na hasira kufuatia hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jesrusalem kama makao makuu ya Israel.

Maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutambua Jerusalem kama makao makuu ya Israel pia yalisuhudiwa katika nchi mbalimbali za Kiarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.