Pata taarifa kuu
IRAN-ISRAEL-PALESTINA-MAREKANI-USALAMA

Rohani: Uamuzi juu ya Jerusalem utaleta maafa katika kanda ya Mashariki ya Kati

Hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake katika mji wa Jerusalemu na kutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel itasababisha janga kwa eneo hilo, amesema leo Jumanne Rais wa Iran, Hassan Rohani.

Rais wa Iran Hassan Rohani apinga uamuzi wa Marekani juu ya Israel.
Rais wa Iran Hassan Rohani apinga uamuzi wa Marekani juu ya Israel. REUTERS/Stephanie Keith
Matangazo ya kibiashara

"Tunapaswa kusimama dhidi ya uamuzi huu mbaya, tukiushtumu kwa sauti moja, tukisema kwamba hilo haliwezekani," Hassan Rohani amesema katika taarifa uliyorushwa kwenye runinga ya taifa., nchini Uturuki, ambapo atashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kesho Jumatano, mkutano ambao utajadili kuhusu uamuzi wa Marekani juu ya Jerusalem.

Waziri wa Ulinzi wa Iran, Amir Hatami, alisema siku ya Jumatatu kuwa uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli utasababisha kufutwa au kuangamizwa kwa taifa la Israel. Kwa upande wake, afisa mwandamizi wa Kikosi cha jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi cha Iran aliwapiga simu viongozi wa makundi mawili yenye silaha ya Palestina kuwajulisha kuhusu kuungwa mkono na nchi yake.

"Kutokana na uamuzi huu usiofaa, mbaya na usio halali, Waislamu walikaa kimya (...)," alisema.

"Ni mtihani kwa Waislamu na ulimwengu wa Kiislam kwa ujumla, pamoja na Wapalestina," aliuongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.