rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Lebanoni Misri

Imechapishwa • Imehaririwa

Saad Hariri asubiriwa Misri Jumanne hii

media
Saad Hariri, Waziri Mkuu Lebanon aliejiuzulu i, bado mabango yenye picha yake yapo Beirut (Novemba 13). REUTERS/Mohamed Azakir

Saad Hariri alitangaza kujiuzulu Novemba 4 wakati alipokuwa nchini Saudi Arabia, akisema kuwa anahofia maisha yake.


Saad Hariri yupo nchini Ufaransa tangu siku ya Jumamosi, ambapo alikutana kwa mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Aliahidi kurudi Lebanoni kushiriki katika sikukuu ya kitaifa siku ya Jumatano.

Saad Hariri amekua akishtumu wanamgambo wa Hezbollah na Iran kuhusika katika mdodoro wa usalama katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Awali rais wa Lebanon, Michel Aoun alitangaza kwamba Bw. Hariri anashikiliwa nchini Saudi Arabia, jambo ambalo alikanusha Bw. Hariri mwenyewe na kusema kwamba ni uzushi mtupu. Nchi kadhaa hasa Ufaransa ziliingilia kati baada ya Saad Hariri kutangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake.