Pata taarifa kuu
IRAN-IRAQ-TETEMEKO-MAJANGA

Tetemeko kubwa la ardhi laua watu zaidi ya 350 Iran na Iraq

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 kwenye vipimo vya Richter lilipiga kaskazini mashariki mwa Iraq na maeneo jirani nchini Iran na Uturuki. Ripoti ya mwisho inasema kuwa watu 348 nchini Iran wamepoteza maisha, na sita nchini Iraq. Tetemeo hilo lilitokea siku ya Jumapili.

Des vitrines brisées à Halabja, en Irak, non loin de l'épicentre du séisme du dimanche 12 novembre 2017.
Des vitrines brisées à Halabja, en Irak, non loin de l'épicentre du séisme du dimanche 12 novembre 2017. TWITTER - Osama Golpy/Rudaw/Social Media/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa Baghdad walisikia tetemeko hilo kubwa kwa muda wa sekunde zaidi ya ishirini. Na wakati mwingine zaidi ya sekunde hizo katika maeneo mengine ya Iraq, kwa mujibu wa mashahidi waliohojiwa na shirika la habari la AFP.

Chanzo cha tetemeko hilo kiliorodheshwa siku ya Jumapili jioni na kilikua na kina cha urefu wa kilomita 25 kilomita zaidi ya thelathini kusini magharibi mwa mji wa Halabja, katika eneo la milima la mkoa wa Iraq la Sulaymaniyeh, idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS) imebaini.

Iran imeathirika zaidi na tetemeko hilo, ambapo watu zaidi ya mia moja wamepoteza maisha. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo idadi ya vifo imeendelea kuongezeka usiku na sasa imefikiwa watu 348 ambao wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 1000 kujeruhiwa.

Miji iliyoathirika zaidi ni Qasr-e Shirin, kwenye mpaka, na Azgaleh. "Tunaweka makambi matatu ya dharura" katika eneo hili, Naibu mkuu wa mkoa wa Kermanshah ameiambia televisheni ya serikali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, timu 30 za maafisa wa uwokoaji kuwaokoa kutoka sirika la kihisabi la Iran zimepelekwa kaskazini mwa Iran. Lakini zoezi hilo linaonekana kuwa ngumu, barabara zimeharibika.

Kulingana na tovuti ya redio na televisheni vya serikali, shule zitafungwa leo Jumatatu katika mikoa ya Kermanshah na Ilam.

Nchini Iraq, watu sita wameripotiwa kupoteza maisha katika mkoa wa Sulaymaniyah katika katika eneo la Kurdistan nchini Iraq, mamlaka imesema.

Katika maeneo mengine ya nchi zote mbili umeme umekata. Na wakazi walitakiwa kulala nje ya nyumba zao kama tahadhari.

Nchini Uturuki, ambapo tetemeko hilo lilisikika, hakuna uharibifu wowote ambao umeripotiwa, kulingana na mamlaka.

Tetemeko kuu la mwisho nchini Iran lilitokea manamo mwezi Desemba mwaka 2003 mjini Bam, katika mkoa wa Kerman, kuelekea kusini mashariki. Watu wasiopungua 31,000 walipoteza maisha na mji huo uliharibiwa kabisa. Mnamo mwezi Juni 1990, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 kwenye vipimo vya Richter nchini Iran karibu na Bahari ya Caspian liliuawa watu 40,000, zaidi ya 300,000 kujeruhiwa na 500,000 waliachwa bila makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.