Pata taarifa kuu
IRAQ-KURDISTAN-USALAMA

Kiongozi wa Kurdistan ajiuzulu, mapambano kuhusu uhuru yaendelea

Kiongozi wa Kurdistan Massoud Barzani haitaendelea kuongoza eneo hilo linalojitawala la Iraq. Saa chache baada ya Bw. Barzani kutangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo siku ya Jumapili usiku, 29 Oktoba, makabiliano yalitokea mbele ya bunge ambapo kilikua kukijadiliwa kwa siku nzima hatua ya ya kuchukua ili kugawanya madaraka ya urais kati ya serikali, Bunge na Mahakama Kuu.

Massoud Barzani wakati wa mkutano katika mji wa Erbil mnamo mwezi Septemba 2017.
Massoud Barzani wakati wa mkutano katika mji wa Erbil mnamo mwezi Septemba 2017. REUTERS/Azad Lashkari/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Eneo la Kurdistan linaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu, wakati ambapo wanasiasa wenyewe wakijitahidi kutafuta njia ya kufanya kazi kwa pamoja.

Massoud Barzani ameacha wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake. Mbelea ya umati wa waandishi wa habari Omed Khoshnaw, mmoja wa vigogo wa chama cha PDK, chama cha Massoud Barzani alijaribukuwahakikishi Wakurdi kwamba "Massoud Barzani bado hata hivyo ni kiongozi wa kihistoria wa Kurdistan. Ataendelea kuhudumu kama mtu kutoka jamii ya Wapeshmerga. Inabidi mfahamu kwamba, ataendelea mpaka Wakurdi wanafikia ushindi wa jumla. "

Hata hivyo, ushindi unaonekana kuwa mbali mbali, ambapo mwezi mmoja uliopita Massoud Barzani alionekana kama kiongozi wa harakati za uhuru, leo baada ya miaka 12 katika uongozi wa wa eneo la Kurdistan nchini Iraq, anaonekana kuwa ameshindwa katika nyanja mbalimbali, kwa mujibu wa mbunge kutoka kambi ya upinzani Rabun Maruf . "Bw. Massoud Barzani alisema anataka kuunganisha vikosi viwili vya Wapeshmerga vilivyojigawa, lakini leo bado tuna vikosi viwili Vya Wapeshemerga vilivyogawanyika. Alisema anataka kuunganisha serikali ya Kurdistan na alikiri mwenyewe kuwa hawezi kufanya hivyo. Alidai kuwa anataka kufanya uchumi wa Kurdistan kujitegemea, kwamba mafuta yaweze tu kubaki Kurdistan. Taarifa rasmi zinasema kwamba mapipa milioni moja ya mafuta yamekua yakivuka mpaka wa Kurdistan kila siku. Lakini zawadi ya uhuru huu wa kiuchumi imekuwa kukata mishahara ya watumishi wa umma kwa 60%. Leo, baada ya kupoteza eneo la Kirkuk, serikali, sera ya Bw. Barzani na mamlaka ya vyama viwili vya PUK na KDP wanahusika na hali ambayo watu wa Kikurdi wanaendelea kukabiliana nayo. "

Wakurdi walikipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria.

Kisha jeshi la Iraq likaanzisha oparesheni ya kuukomboa mji uliokuwa chini ya wakurdi wa Kirkuk na kuteka vituo vya mafuta vya mji huo.

Bwana Barzani alisema atasalia mpiganiaji wa kurdi na atazidi kutetea mafanikio ya watu wa Kurdistan.

Bw Barzani aliingia ofisini mwaka 2005 baada ya kuhusika katika wajibu mkubwa wa kunda eneo huru la Kurdistan lililo kaskazini mwa Iraq baada ya Saddan Hussen kuondolewa madarakani.

Bw. Barzani alichukua uamuzi huu wa kuandaa kura ya maoni bila kushirikisha wengine na hali hiyo ikapelekea upande mwengine ambao ni mshirika wa mamlaka ya Kikurdi (PUK) kutafakari upya msimamo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.