rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iraq

Imechapishwa • Imehaririwa

Majeshi ya Iraq yaingia Kirkuk, waasi wa Kikurdi watimka

media
Vikosi vya Iraq katika mji wa Kirkuk, Oktoba 16, 2017. REUTERS

Majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuingia katikati ya mji wa Kirkuk, linalodhibitiwa na wapiganaji wa Kikurdi ambao wanaripotiwa kutoroka.


Pamoja na wapiganaji hao, maelfu ya raia wa kawaida pia wameyakimbia makwao kwa hofu ya mapigano.

Iraq inasema lengo la jeshi ni kudhibiti eneo hilo ambalo lilishiriki katika kura ya maoni kutaka kujitawala lakini pia kuwaondoa wapiganaji wa Islamic State.

Awali serikali ya Baghdad ilisema askari wa Iraq wana majukumu ya "kutoa ulnzi katika kambi za jeshi na visima vya mafuta katika mkoa wa Kirkuk". Katika mji huo, Gavana wa Kikurdi, alifutwa kazi na serikali kuu ya Baghdad lakini alikataa kuacha nafasi yake, na hivyo kutolewa wito wakazi wa mji huo kuchukua silaha kulinda mji wao.

Jumapili, Oktoba 15, viongozi wa Kikurdi walisema wako tayari kuzungumza na serikali kuu ya Baghdad lakini walipinga wazo la kufuta kura ya maoni ya uhuru kama sharti la mazungumzo yoyote na Baghdad.

Muda mfupi baadaye, serikali ya Iraq ilibadili kauli yake na kushtumu uwepo wa wapiganaji wa Kikurdi kutoka Uturuki katika mkoa wa Kirkuk na kusema kuwa waliona "tangazo la vita".

Siku ya Jumatatu mrekani iliwataka viongozi wa Iraq na viongozi wa eneo la Kikurdi kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu za kiusalama.