rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Afghanistani Taliban

Imechapishwa • Imehaririwa

Kambi kubwa ya polisi ya Gardez, Afghanistan yashambuliwa

media
Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika eneo la shambulio la kituo cha polisi cha Gardez tarehe 18 Juni 2017. AFP

Kambi kubwa ya polisi ya Gardez, ikiwa ni pamoja na kituo cha mafunzo, kusini mashariki mwa Afghanistan, imeshambuliwa Jumanne hii na wapiganaji wa Taliban, ambao wameingia ndani ya jengo hilo baada ya kulipua gari moja au mbili, vyanzo rasmi vimeripoti.


Kundi la Taliban, kupitia ujumbe wa msemaji wake Zabiullah Mujahid kwenye twitter, limedai kutekeleza shambulio hilo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan, katika taarifa yake, imebaini kwamba shambulio hilo bado limekua likiendelea saa 10:30 saa za Afghanistan (sawa na saa 06:00 saa za kimataifa), zaidi ya saa baada ya milipuko ya kwanza. "Washambuliaji waliovalia mikanda iliyojaa vilipuzi wamelipua gari moja iliyokua imetegwa bomu na kisha kundi la magaidi lilingia katika jengo hilo, " taarifa ya wizara imesema

Allah Mir Bahram, mjumbe wa baraza la mkoa wa Paktiya, linalopakana na maeneo yenye mizozo ya Pakistan, ameiiambia shirika la habari la AFP kwamba "magari mawili yaliyotehwa mabomu" yalilipuka mbele ya lango kuu la jengo hilo.

Vikosi maalum imezingira kambi hiyo idadi kubwa ya polisi imetumwa katika eneo hilo, wizara imeongeza.

Mbali na kituo cha mafunzo, kambi ya Gardez inahifadhi, kikosi cha polisi ya taifa, polisi wa mpaka na kikosi cha askari.