Pata taarifa kuu
IRAQ-KURDISTAN-USALAMA

Mapigano makali yarindima katika mkoa wa Kirkuk

Vita vikali vimezuka katio ya majeshi ya Iraq na wapiganaji wa Kikurdi katika mkoa wa Kirkuk, kaskazini mwa nchi hiyo.

Mafuta ni chanzo cha mgogoro kati ya Baghdad na Wakurdi: malori ya mafuta yakisubiri kusafirisha mafuta kwenyekisima cha mafuta Kirkuk, katika eneo la Kurdistan nchini Iraq (Picha ya zamani).
Mafuta ni chanzo cha mgogoro kati ya Baghdad na Wakurdi: malori ya mafuta yakisubiri kusafirisha mafuta kwenyekisima cha mafuta Kirkuk, katika eneo la Kurdistan nchini Iraq (Picha ya zamani). Photo by Staton R Winter/Bloomberg via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku tatu, serikali ya Iraq imekuwa ikiomba Wapeshmergas wa Kikurdi kuondoka kutoka mji wa Kirkuk na kufuta kura ya maoni ya uhuru ya tarehe 25 Septemba. Hatimaye mapigano yalizuka kati ya askari wa Iraq na wapiganaji wa Kikurdi (peshmerga) usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu na hii Jumatatu na Jumatatu hii asubuhi majeshi ya Iraq yamehakikisha kuwa yanadhibiti barabara na miundombinu karibu na Kirkuk.

Vyanzo vya kijeshi kwa pande zote mbili vinasema urushianaji makombora, kusini mwa Kirkuk, umesababisha watu kadhaa kujeruhiwa katika safu ya wapiganaji wa Kikurdi (peshmerga).

Serikali ya Baghdad imesema askari wa Iraq wana majukumu ya "kutoa ulnzi katika kambi za jeshi na visima vya mafuta katika mkoa wa Kirkuk". Katika mji huo, Gavana wa Kikurdi, alifutwa kazi na serikali kuu ya Baghdad lakini alikataa kuacha nafasi yake, na hivyo kutolewa wito wakazi wa mji huo kuchukua silaha kulinda mji wao.

Maafisa usalama wa Kikurdi wamesema majeshi ya Iraq yanalenga kushika udhibiti kwenye eneo hilo lenye mafuta na kuliko pia na kambi ya anga ya K1q

Jumapili, Oktoba 15, viongozi wa Kikurdi walisema wako tayari kuzungumza na serikali kuu ya Baghdad lakini walipinga wazo la kufuta kura ya maoni ya uhuru kama sharti la mazungumzo yoyote na Baghdad.

Muda mfupi baadaye, serikali ya Iraq ilibadili kauli yake na kushtumu uwepo wa wapiganaji wa Kikurdi kutoka Uturuki katika mkoa wa Kirkuk na kusema kuwa waliona "tangazo la vita".

Marekani inataka mazungumzo kati ya viongozi wa Iraq na eneo la Kikurdi kwa sababu za kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.