rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iraq Haidar al Abadi Ufaransa Emmanuel Macron

Imechapishwa • Imehaririwa

Al-Abadi atoa wito kwa utulivu, Macron ataka haki za Wakurdi zihesimishwe

media
Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika ikulu ya Elysée, Paris tarehe 5 Oktoba 2017. REUTERS/Ludovic Marin/Pool

Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi yuko zirani nchini Ufaransa.Hayo yanajiri wakati ambapo kundi la Islamic State linaendelea kushindwa kila kukicha katika uwanja wa vita nchini humo, huku nchi hii ikikabiliwa na mvutano mpya kufuatia kura ya kujitawala kwa eneo la Kurdistan ya Septemba 25.


Waziri Mkuu wa Iraq amekutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Suala la Wakurdi na vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu limetawala mazungumzo yao.

Haidar al-Abadi amesema hakua anataka "makabiliano ya kijeshi" na eneo la Kurdistan, ambalo hivi karibuni, lilipiga kura ya kujitawala, na ametolea wito wapiganaji wa Kikurdi wa (Peshmerga) kuendelea kupambana upande wa vikosi vya Iraq . "Hatutaki mapigano, lakini mamlaka ya shirikisho yatatathmini hali hiyo," amesema Waziri Mkuu wa Iraq baada ya kukutana kwa mazungumzo mjini Paris na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

"Ninatolea wito Wapeshmerga kushirikiana nasi kama tulivyoshirikiana pamoja dhidi kundi la Islamic State, kwa kuhakikisha usalama wa raia wetu," amesisitiza Waziri Mkuu wa Iraq, huku akirejelea kwamba "kujiondoa" kwa Eneo la Kurdistan "haikubaliki ".

Kura ya maoni kuhusu uhuru wa Kurdistan nchini Iraq, iliyopitishwa tarehe 25 Septemba kwa idadi kubwa kura, imesababisha mgogoro mkubwa kati ya serikali kuu ya Baghdad na eneo la Kurdistan, ambapo tangu wakati huo linakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi kutoka serikali kuu lakini pia majirani zake Uturuki na Iran, wanaopinga jaribio lolote la kujitawala kwa eno la Kurdistan.

Mgogoro huu unakuja wakati ambapo Iraq imekua ikifaulu katika vita vyake vya kurejesha kwenye himaya yake ngome zote za kundi la Islamic State, vita ambavyowapiganaji wa Kikurdi (Peshmerga) wako kwenye mstari wa mbele. Haidar al-Abadi pia ametangaza rasmi kwa majeshi yake yamefaulu "kuukomboa" mji wa Hawija, moja ya ngome ya mwisho ya kundi la Islamic State.

"Ushirikiano Kamili" wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa amemwambia mwenzake wa Iraq "msaada kamili" wa Ufaransa katika muungano unaopambana dhidi ya kundi la Islamic State. "Tutaendelea hadi mwisho na kwa muda mrefu kama itahitajika sisi kuwepo," amesema Emmanuel Macron, huku akiahidi kufungua "ukurasa mpya katika uhusiano wa nchi hizo mbili" kati ya Ufaransa naIraq.

Akizungumzia mgogoro wa eneo la Kurdistan, rais wa Ufaransa amesema kuwa Paris imekua ikitaka "utulivu wa Iraq, uheshimishwaji wa mipaka ya Iraq na serikali yenye nguvu nchini Iraq." Lakini pia amesisitiza kuwa Ufaransa inaendelea kuwa na "wasiwasi kuhusu hali ya Wakurdi". "Tunaomba haki za Wakurdi zitambuliwe katika Katiba ya Iraq," (iliyopipitishwa mwaka 2005), amesema Emmanuel Macron.