Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-IS-USALAMA

Shambulio la IS laua watu sita Kabul

Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio la kujitoa mhanga lililowaua wati sita kutoka jamii ya Mashia na wengine zaidi ya thelathini kujeruhiwa. Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa mbele ya msikiti wa Kishia katikati ya mji wa Kabul wakati wa sherehe za kidini.

Polisi ya Afghanistan baada ya shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya Msikiti wa Kishia Septemba 29, 2017 Kabul.
Polisi ya Afghanistan baada ya shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya Msikiti wa Kishia Septemba 29, 2017 Kabul. AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa inaweza kuongezeka, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, huku ikibaini kwamba watuhumiwa watatu wamekamatwa .

"Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijaribu kujilipua na kusababisha vifo vya watu sita, mita 140 kutoka Msikiti wa Mashia wa Hussainia" katika eneo la makazi la Qala-e-Fatullah, Mkuu wa polisi, Salim Almas ameliambia shirika la habari la AFP, akisema kuwa watu sita wameuawa na 16 wamejeruhiwa.

Kwa upande wake, shirika lisilo la kiserikali kutoka Italia, ambalo lina hospotali kubwa katika mji wa Kabul, limesema katika Twitter kwamba limepokea majeruhi 33 na watoto sita."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Denmark Najib ametangaza kukamatwa kwa "watuhumiwa wengine watatu, ambao bado wanazuiliwa katika eneo la tukio."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.