Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

30 waangamia katika mlipuko mskitini nchini Afghanistan

Watu wasiojulikana wameendesha shambulio dhidi ya Msikiti wa Jawadia katika mji wa Herat, magharibi mwa Afghanistan kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa vyanzo ya usalama.

Shambulizi dhidi ya Msikiti wa Kishia wa Herat lilifanyika muda mfupi kabla ya sala ya jioni, Jumanne, Agosti 1, 2017.
Shambulizi dhidi ya Msikiti wa Kishia wa Herat lilifanyika muda mfupi kabla ya sala ya jioni, Jumanne, Agosti 1, 2017. REUTERS/Mohammad Shoib
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa hakuna kundi linalodai kuhusika na shambulio hilo. Milipuko na risasi nyingi zilifyatuliwa ndani ya Msikiti huo. Haijajulikana na ni sababu zipi zilizopelekekea Msikiti huo kushambuliwa.

Msemaji wa polisi katika eneo la Herat amesema shambulio hilo limetekelezwa na mlipuaji wa kujitoa muhanga.

Shambulio dhidi ya Mskiti wa Jawadia limetokea saa mbili usiku siku ya Jumanne kuamkia Jumatano wakati mamia ya waumini walipokuwa wanaswali swala ya jioni.

Mskiti huo upo katika eneo la mji wa Herat ulio na idadi kubwa ya wasilamu wa madhehebu ya Shia.

Herat, mji uliopo karibu na mpaka na Iran, unatazamwa kuwa mojawapo ya miji ya amani nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.