Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Israel yaondoa vifaa vya usalama kwenye eneo takatifu la Jerusalem

Serikali ya Israel imetangaza kuondoa vifaa maalumu vya ukaguzi kwenye eneo takatifu la msikiti wa Jerusalem, ikisema haitatumia tena vifaa hivyo baada ya kuzusha sintofahamu mwishoni mwa juma kati ya waumini na vikosi vya Serikali.

Wafanyakazi wa Israel wakiondoa vifaa maalumu vya ukaguzi kwenye msikiti wa Al-Aqsa. Juni 25, 2017
Wafanyakazi wa Israel wakiondoa vifaa maalumu vya ukaguzi kwenye msikiti wa Al-Aqsa. Juni 25, 2017 REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umekuja wakati huu jumuiya ya kimataifa ilikuwa inafanya juhudi kuzuia vurugu kwenye ardhi ya Palestina, huku utawala wa Israel ukisema utatumia mbinu nyingine za kiusalama baada ya juma moja lililopita wanajeshi wake wawili kuuawa kwenye msikiti wa Al-Aqsa.

Maofisa wa kiislamu bado hawajaamua ikiwa wakubaliane na hatua ya Israel au la ili wasitishe mgomo wao wa kutotumia msikiti huo kusalia ambao unatumiwa pia kama kanisa na raia wa kiyahudi.

Timu maalumu ilifanya kazi ya kuondoa vifaa maalumu vya utambuzi kwenye geti kuu la kuingilia kwenye msikiti huo na hata kamera zilizokuwa zimewekwa kwenye eneo hilo pia nazo ziliondolewa.

Mamia ya wanajeshi wa Israel hata hivyo walisalia kwenye lango kuu la kuingilia kwenye msikiti huo, eneo ambalo waumini wa kiislamu kwa karibu juma moja wamekuwa wakisali nje ya lango la kuingilia.

Vyombo vya usalama vya Israel vilichukua aumuzi wa kuondoa mitambo hiyo alfajiri ya kuamkia siku ya Jumanne.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema kuwa vyombo vya usalama sasa vimeamua kuondoa mitambo hiyo na badala yake kutafanyika ukaguzi wa kawaida kwa waumini wote wanaoingia kusali kwenye eneo hilo takatifu.

Baada ya tangazo hili la Serikali raia kadhaa wa Palestina walijitokeza kushangilia nje ya lango la kuingilia kwenye eneo hilo kama ishara ya ushindi, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa kipalestina waliojaribu kufyatua fataki.

Hata hivyo mamlaka za Israel hazijaweka wazi teknolojia mpya itakayotumika kulinda usalama wa eneo hilo.

Israel iliweka mitambo maalumu kwenye lango la kuingilia kwenye msikiti huo wa Al-Aqsa July 14 mwaka huu saa chache baada ya askari wake wawili kuuawa na mtu mwenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.