Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-USALAMA

Mji wa Mosul wakombolewa kutoka mikononi mwa IS

Mapigano makali yaliokua yakishuhudiwa katika kipindi cha miezi tisa wakati wa vita vya kuukomboa mjio wa Mosul, nchini Iraq yamemalizika Jumapili hii, Julai 9.

Picha ambapo anaonekana Waziri Mkuu Haidar al-Abadi (katikati) akiwasili Mosul Jumapili hii, Julai 9, 2017.
Picha ambapo anaonekana Waziri Mkuu Haidar al-Abadi (katikati) akiwasili Mosul Jumapili hii, Julai 9, 2017. REUTERS TV/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mapema mchana, Waziri Mkuu wa Iraq, Haidar al-Abadi aliwasili "katika mji huo uliokombolewa na kupongeza wapiganaji mashujaa na wananchi wa Iraq kwa ushindi huo mkubwa," ilisema taarifa kutoka ofisi yake.

Kukombolewa kwa mji wa Mosul ni moja ya njia ya kumalizi kwa mapigano yalioanzishwa mwezi Oktoba na vikosi vya Iraq, vikiungwa mkono na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani. Kundi la Islamic State lilikua liliufanya mji wa Mosul kama ngome yake kuu nchini Iraq. Katikati mwa mwezi Juni mwaka 2014, katika msikiti wa Al-Nouri, kiongozi wa ISlamic State, Abu Bakr al-Baghdadi alitangaza kuwa kiongozi wa kiislamu katika eneo lote wapiganaji wa Islamic State wanalodhibiti"Ukhalifa" kutoka kubwa al-Nouri msikiti, katikati ya Juni, 2014.

Huu ni ushindi muhimu zaidi wa Iraq dhidi ya kundi la IS tangu kundi la Masunikuvamia mwaka huo maeneo makubwa ya Iraq. Hata hivyo, wapiganaji wa kundi la Islamic State bado wakp magharibi na kusini mwa mji huo.

Mji uliharibiwa

Toka siku Jumamosi, bila kusubiri tangazo rasmi, askari kadhaa wa Iraq walikuwa wameanza kusherehekea ushindi, wakicheza na kufyatua risasi. vyanzo nchini Iraq vinadai kuwa wakati kukombolewa kwa Mosul ni hatua ya mwisho katika vita hivyo nchini Iraq.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukarabati wa miundombinu muhimu utagharimu pengine zaidi ya dola bilioni moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.