Pata taarifa kuu
SAUDI-ARABIA-QATAR-USHIRIKIANO

Saudi Arabia na washirika wake kuendelea kuitenga Qatar

Mawaziri wa kigeni wa nchi nne ambazo zimeitenga Qatar, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain walikutana Cairo siku ya Jumatano Julai 5 kujadili athari za hatua dhidi ya nchi hiyo.

Mawaziri wa kigeni wa Saudi Arabia Abdelal-Jubeir (wa pili kutoka kushoto), Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed al Nahyan (kushoto), Misri Sameh Chroukry (kulia) na Bahrain Khalid bin Ahmed al- Khalifa (wa pili kutoka kulia), Cairo, Julai 5, 2017.
Mawaziri wa kigeni wa Saudi Arabia Abdelal-Jubeir (wa pili kutoka kushoto), Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed al Nahyan (kushoto), Misri Sameh Chroukry (kulia) na Bahrain Khalid bin Ahmed al- Khalifa (wa pili kutoka kulia), Cairo, Julai 5, 2017. REUTERS/Khaled Elfiqi
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja, walisema watadumisha vipimo vya "kuitenga Qatar kama itaendelea na uungwaji wake mkonona msimamo mkali na ugaidi. mkutano mpya Umepangwa kufanyika Manama nchini Bahrain.

Taarifa ya nchi hizi nne inasema hakuna hoja ya kuondoa vikwazo dhidi ya Qatar. Nchi hizi nne zinaonyesha kwamba hakuna suala la kuondoa vikwazo dhidi ya Qatar kama nchi imekubali kushiriki katika mapambano dhidi ya siasa kali na ugaidi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar anataka kufanyika kwa mazungumzo na mataifa mengine ya kiarabu ili kumaliza mvutano unaondelea.

Waziri huyo Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amesema mazungumzo pekee ndio yanayoweza kutatua mvutano huu wa madai kuwa inaunga mkono ugaidi na kusema ni hatua ya kujaribu kuingilia uhuru wa nchi yake.

Wito huu umekuja Mawaziri wanne wa mataifa ya kiarabu wakikutana jijini Cairo nchini Misri, kuamua kuichukulia Qatar hatua zaidi.

Mataifa hayo yalikuwa yametia saa 48 kwa Qatar kufunga kitruo chake cha Aljazeera katika mataufa hayo kwa madai kuwa kinatumiwa kufadhili ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.