Pata taarifa kuu
QATAR-UGAIDI

Mauritania na Gabon zaunga mkono kutengwa kwa Qatar

Mauritania na Gabon yameungana na Libya na Misri kutoka barani Afrika, kuunga mkono hatua ya Qatar kutengwa na mataifa ya kiarabu kwa madai ya kuunga mkono makundi ya kigaidi.

Shirika la ndege la Qatar
Shirika la ndege la Qatar Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Mauritania amesema sera za Qatar zinaunga mkono wazi makundi ya kijihadi ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

'Sera za Qatar zinaunga mkono makundi ya kigaidi,” Imesema taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje.

Gabon ambayo inafahamika kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika, imeishtumu Qatar imeshindwa kuheshimu sheria za Kimataifa kupambana na ugaidi.

Aidha, Wizara ya Mambo ya nje ya nchi hiyo imesema Qatar kwa muda mrefu imeendelea kuyaunga mkono makundi ya waasi.

Wakati uo huo, rais wa Marekani Donald Trump ameyataka mataifa ya Ghuba kuungana katika vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali, baada ya kuusifu msimamo wa Saudi Arabia.

Trump ametoa kauli hii baada ya kumpigia simu Mfalme Salman wa Saudi Arabia na kumhakikishia kuwa anaunga mkono hatua ambayo ilichukuliwa na mataifa kadhaa ya kiarabu kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia na Qatar kwa mada kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.

Qatar imekanusha madai hayo na kusema hakuna ushahidi kuonesha kuwa inaunga mkono ugaidi.

Saudi Arabia imesitisha safari za ndege kati ya nchi hizo mbili huku Bahrain ikitaka raia wa Qatar kuondoka nchini humo kwa muda wa siku 14.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.