rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Yemeni Marekani Al Qaeda

Imechapishwa • Imehaririwa

Washukiwa watano wa Al qaeda wauawa Yemen

media
Washukiwa watano wa kundi la Al Qaeda wauawa Yemen REUTERS/Naif Rahma

Washukiwa watano wa tawi la kigaidi la Al-Qaeda nchini Yemen wameuawa jumapili katika kile kinachoelezwa na mamlaka kuwa shambulizi la anga lililotekelezwa na ndege za Marekani mashariki mwa jiji la Sanaa.


Shambulizi la mapema jumapili lililenga gari lililokuwa likisafirisha silaha katikati mwa jimbo la Marib kutoka Yakla jimboni Baida,kwa mujibu wa jeshi.

Maafisa wamesema gari lilikuwa linamilikiwa na kiongozi mmoja wa Al-Qaeda katika ghuba ya kiarabu ambayo Marekani inalitaja kuwa tawi hatari zaidi lenye msimamo mkali.

Shambulizi la jumapili linakija ikiwa ni masaa 24 kupita baada ya kutekelezwa shambulizi kama hilo lililoua wanamgambo 3 kusini mwa jimbo la Shabwa ambalo limelengwa zaidi na vikosi vya Marekani.