rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Afghanistani Taliban

Imechapishwa • Imehaririwa

Askari zaidi ya 50 wa Afghanistan wauawa katika shambulizi

media
Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikiwasili kwenye eneo la shambulizi, karibu na mji wa Mazar-e-Sharif katika jimbo la Balkh kaskazini mwa Afghanistan, Aprili 21, 2017. FARSHAD USYAN / AFP

Askari wasiopungua 50 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi la Afghanistan kaskazini mwa nchi, karibu na mji wa Mazar-e-Sharif. Shambulizi hilo lililodumu saa kadhaa limemalizika mapema jioni, kwa mujibu wa jeshi la Marekani.


"Askari zaidi ya 50 wa Afghanistan wameuawa" katika shambulizi dhidi ya kambi yao, shambulizi ambalo lilieneshwa na kundi la Taliban siku ya Ijumaa karibu na mji mkubwa wa kaskazini wa Mazar-e-Sharif, msemaji wa jeshi la Marekani mjini Kabul ameliambia shirika la habari la AFP mapema siku ya Ijumaa jioni.

Shambulizi hilo limetokea katika kambi ya Mazar-e-Sharif, mji mkuu wa mkoa wa Balkh, wakati ambapo askari walikuwa wakitokea msikitini baada ya sala ya Ijumaa.

Katika taarifa yake, afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani ,John Nicholson, ambaye anaongoza operesheni ya muungano wa majeshi ya kujihami ya Magharibi NATO ya Resolute Support, amesema kuwa shambulizi lililenga "watu wakati wa sala msikitini na wengine katika chumba cha kulia" katika kambi ya 209TH ya jeshi la Afghanistan, karibu na mji wa Mazar.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan, Dawlat Waziri, aliyehojiwa mapema na shirika la habari la AFP, shambulizi lilitokea mapema mchana, liliendeshwa na kundi la watu wenye silaha ambao walikua wamevalia sare.

Shambulio hilo limedaiwa na kundi la Taliban katika taarifa yake: "kwenye saa 8 (sawa na saa 3:30 asubuhi saa za kimataifa), wapiganaji wetu walitekeleza shambulizi kubwa dhidi ya jeshi katika mji wa Mazar-e-Sharif katika jimbo la Balkh, na kusababisha vifo vya askari wengi, "ameandika msemaji wao Zabihullah Mujahib, akinukuliwa na shirika la habari la AFP.