rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Afghanistani Taliban

Imechapishwa • Imehaririwa

Mmoja wa viongozi wa Taliban kaskazini mwa Afghanistan auawa

media
Mpiganaji wa Taliban katika mitaa ya Kunduz, ambapo wapiganaji wa Afghanistan walichukua udhibiti tarehe 28 Septemba. REUTERS/Stringer

Kiongozi wa Taliban katika mkoa wa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan ameuawa. Kifo chake kimethibitishwa na kundi la Taliban. Kiongozi huyo aliuawa na ndege isio na rubani. Alikua mmoja wa wapiganaji wa Taliban walioteka kwa muda kwa mara ya kwanza mji wa Kunduz mwaka 2015.


Hii si mara ya kwanza kifo cha Abdul Salam Akhund kutangaza. Lakini wakati huu taarifa imethibitishwa na Msemaji wa kundi la Taliban. Msemaji wa Taliban anasema kuwa Abdul Salim aliuawa Jumapili kwa makombora yaliyorushwa na ndege isio na rubani ya Marekani wakati ambapo alikua wilayani Archi kaskazini mwa mkoa wa Kunduz.

Shambulizi hilo limethibitishwa na jeshi la Marekani, ambalo halijasungumzia idadi ya waliouawa katyika shambulizi hilo. Hata hivyo viongozi wa serikali za mitaa wamearifu kwamba, wapiganaji tisa wa Taliban waliuawa wakati wa operesheni hiyo.

Aidha, ripoti zinasema kuwa pamoja na Kamanda huyo, wapiganaji wengine watatu wa kundi hilo wameuawa baada ya kushambuliwa.