Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watu zaidi ya 30 waangamia katika mashambulizi mawili mjini Kabul

Watu wasiopungua thelathini wameuawa na wengine zaidi ya themanini wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyotokea Jumanne hii Januari 10 katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Kundi la Taliban limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Afisa wa polisi apelekwa hospitalini baada ya mashambulizi mawili katika mji wa Kabul Jumanne, Januari 10, 2017.
Afisa wa polisi apelekwa hospitalini baada ya mashambulizi mawili katika mji wa Kabul Jumanne, Januari 10, 2017. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe uliyorushwa kwenye mtandao wa Twitter, kundi la Taliban limekiri kuwa lililenga basi ndogo iliyokua ikiwasafirisha maafisa wa Ofisi ya Kitaifa ya Usalama, Idara ya kuu ya Ujasusi nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, mlipuko wa kwanza ulitokea mbele ya basi la abiria lililokua likisubiri watu ambao walikua wakitokea katika jengo la Bunge jipya. Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliwasogelea maafisa wa usalama waliokua wakiondoka katika ofisi yao na kulipua mkanda uliyokua umejaa vilipuzi katikati ya umati wa watu. Dakika chache baadaye, gari jingine ndogo liliegeshwa upande wa pili wa barabara na kulipuka.

Mashambulizi haya mawili yalitokea saa moja kabla ya maafisa kuondoka kazini wakirudi nyumbani, katika kata inayotembelea na watu wengi mjini kabul. Katika eneo hili kumejengwa majengo mbalimbali ya serikali, ikiwa ni pamoja na jengo la Bunge jipya, lakini pia Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul, ambacho kilishambuliwa mwezi Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu wengi.

Mwezi mmoja baadaye, mwishoni mwa mwezi Novemba, msikiti wa Kishia katika mji wa Kabul, ulilengwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga. watu thelathini waliuawa. Kundi la Islamic State lilidai kutekeleza shambulizi hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.