Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI-USALAMA

Askari wa Afghanistan katika mafunzo Marekani watoroka jeshi

Askari arobaini na nne wa Afghanistan wametoweka tangu mwezi Januari 2015 wakati wa mafunzo ya kozi nchini Marekani, na inashukiwa kuwa huenda wameamua kuishi nchini humo kinyume cha sheria, Pentagon imesema.

Askari wa Afghanista wakipewa mafunzo ya kijeshi mjini Kabul mwaka 2001.
Askari wa Afghanista wakipewa mafunzo ya kijeshi mjini Kabul mwaka 2001. (Photo : S. Malibeaux/RFI).
Matangazo ya kibiashara

Jumla ya askari 2,200 wa jeshi la Afghanistan walipewa mafunzo ya jeshi tangu mwaka 2007. Askari wengine wa kigeni walipata nafasi hiyo kwa kulitoroka jeshi, lakini kwa askari wa Afghanistan ni jambo la 'kawaida', chanzo cha wizara ya ulinzi ya Marekani kinatambua hilo.

Tangu mwezi Septemba, askari wanane waliondoka katika kambi za jeshi la Marekani bila ruhusa, amesema Adam Stump, msemaji wa Pentagon, akihojiwa na shirika la utangazaji la Reuters.

"Wizara ya Ulinzi inatathimini njia mbadala ya kuongeza vigezo (uteuzi) kwa ajili ya mafunzo ili kupunguza hatari ya kulitoroka jeshi nchini Marekani kwa upande wa Afghanistan," Adam Stump ameongeza.

Hakuna kitu kinaonyesha kwamba askari hao watoro walihusika katika shughuli za uhalifu au kwamba ni tishio kwa Marekani, chanzo kimoja kilio karibu na Pentagon kimebaini.

Wapiganaji wa kundi la Taliban wakati mwingine walijiingiza bila kuwatambua katika safu ya jeshi la Afghanistan kwa kuwashambulia askari wa kikosi cha Marekani, lakini kesi ni nadra tangu kupitishwa kwa hatua mpya za kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.