rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

UAE Ajali

Imechapishwa • Imehaririwa

Ndege aina ya Boeing yapata ajali Dubai, uwanja wa ndege wafungwa

media
Mtazamo wa uwanja wa ndege wa Dubai. dubaiairshow.aero

Ndege aina ya Boeing 777 ya shirika la ndege la Emirates iliyokua ikitokea nchini India imefanya ajali Jumatano hii wakati ilipokua ikijaribu kutua katika Dubai uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, na kusababisha uwanja huo kufungwa, lakini abiria wote waliondolewa salama ndani ya ndege, Mmamlaka ya uwanja wa ndege imesema.


Shughuli kwenye uwanja wa ndege wa Dubai, moja ya viwanja vyenye shughuli nyingi duniani, zimepangwa kuanza tena saa 12:30 saa za nchi hiyo (sawa na 8:30 mchana saa za kimataifa) pamoja na "kipaumbele ndege kubwa," imesema kwenye Twitter mamlaka ya uwanja wa ndege wa Dubai .

Shirika la ndege la Emirates, ambalo linamilikiwa na utawala wa kifalme wa Dubai, limetangazakwenye Twitter "tukio" hili ikilihusisha moja ya ndege yake katika uwanja wa ndege, na kuongeza kuwa halijajua bado nini kilichosababisha ajali hiyo.

Mamlaka ya usafiri wa anga katika Umoja wa nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) aimeanzisha uchunguzi kujua sababu za ajali "kwa ushirikiano na shirika la ndege la Emirates pamojana mamlaka ya uwanja wa ndege."