Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO

Waasi wa Aleppo washindwa kuvitimua vikosi vya serikali

Waasi wa Syria wameshindwa Jumapili hii kufungu upya barabara inayowapa fursa ya kuingiza vifaa na chakula maeneo yao katika mji wa Aleppo (kaskazini), na hivo kupoteza wapiganaji thelathini wakati wa mapigano.

Milio ya risasi na milipuko katika mji wa Allepo, Syria, Julai 9, 2016.
Milio ya risasi na milipuko katika mji wa Allepo, Syria, Julai 9, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi hii usiku wapiganaji hao walizindua mashambulizi kwa lengo la kurejesha udhibiti wa barabara inayoitwa Castello, kaskazini mwa jimbo la Aleppo, ambapo vikosi vya serikali viliweza kudhibiti Alhamisi, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Barabara hii ni muhimu kwa vile ni barabara ya mwisho inayotoa nafasi kwa waasi kuingiza vifaa na chakula katika maeneo wanayoyodhibiti, ambapo wanaishi takriban watu 200,000.

Vikosi vya utawala wa Bashar al-Assad, ambavyo vindhibiti nusu ya jimbo la Aleppo, vinataka kurejesha kwenye himaya yao maebeo yote hayo. Vikosi hivyo vilishambulia kwa mabomu Jumapili hii barabara ya Castello barabara na pembezuni mwake kwa mujibu wa OSDH.

Wapiganaji angalau 29 wa kundi la waasi wa Kiislam la Faylaq al-Cham na mshirika wake Al-Nosra Front (tawi la kundi la Al Qaeda nchini Syria) wameuawa katika mapigano au kwa mabomu ya kutegwa ardhini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.