Pata taarifa kuu
IRAQ-MASHAMBULIZI

Iraq: Siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Serikali ya Iraq imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu hii Julai 4, baada ya watu 119 kuuawa Jumapili hii katika mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliyotekelezwa na kundi la Islamic State. Wengi mwa waliouawa ni raia wa kawaida, vyanzo vya polisi vimetangaza.

Shambulizi baya kabisa, shambulizi la kujitolea muhanga kwa bomu lililotegwa ndani ya gari, limelitikisa eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City kaskazini mwa Baghdad, na kuua watu 21.
Shambulizi baya kabisa, shambulizi la kujitolea muhanga kwa bomu lililotegwa ndani ya gari, limelitikisa eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City kaskazini mwa Baghdad, na kuua watu 21. REUTERS/Khalid al Mousily
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo mawili ya Jumapili hii Julai 3 yalisababisha vifo vya watu 119 na zaidi ya 180 kujeruhiwa katika mji wa Baghdad. Bila kuchelewa kundi la Islamic State lilitangaza kwamba ndio lilihiusika na mashambulizi hayo, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.

Kuanzi Julai 4, siku moja baada yamashambulizi hayo na baada ya matuikio ya kutisha kutokea mwishoni mwa wiki hii iliyopita, siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa na Waziri Mkuu Haider al-Abadi, ambaye alitembelea eneo la tukio na kuahidi "kuwaadhibu" waliohusika kitendo hiki kiovu.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Iraq alitangaza siku ya Jumapili mabadiliko ya hatua za usalama katika mji wa Baghdad, ikiwa ni pamoja na kuondoa vifaa vya kukagua vilipuzi, ambapo serikali inaona kuwa havifanyi kazi.

Bw Abadi pia akiiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kuongeza kasi ya "kupelekwa kwa vifaa vya aina ya Rapiscan ili kutafuta magari yanayotumiwa kwa kuendesha vitendo viovu kwenye barabara zote zinazoingia katika mji wa Baghdad, na kupiga marufuku ya matumizi ya simu za mkononi kwa maafisa wa usalama ambao bado wanafanya kazi. "

Pamoja na msaada wa muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, usalama bado ni tete katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Julai 3, gaidi wa kundi la Islamic State alijilipua mapema asubuhi ndani ya gari lake lililokua lilitegwa bomu katika eneo la kibiashara la Karrada, linalotembelewa na watu wengi kabla ya Siku kuu inayoshiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.