Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN

Watu wasiopungua 22 wauawa katika shambulizi Kabul

Mapema Jumatatu Juni 20, shambulizi lililoendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga lililenga basi katika mji wa Kabul na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 22.

Basi lililolengwa na shambulizi baya Jumatatu, Juni 20, 2016 katika mji wa Kabul, Afghanistan.
Basi lililolengwa na shambulizi baya Jumatatu, Juni 20, 2016 katika mji wa Kabul, Afghanistan. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Gari hili lilikuwa limebeba wafanyakazi wa Usalama kutoka Nepal, maafisa wa Afghanistan wamesema. Kwa uchache watu 14 wameuawa. Watu wengine wanane wamejeruhiwa.

Msemaji wa kundi la wapiganaji wa Taliban amekiri kwenye mitandao ya kijamii kuwa wao ndio wamehusika na shambulizi hilo.

Mshambuliaji alionekana akitembea "kwa miguu", kwa mujibu wa polisi, muda mfupi kabla 12:00 asubuhi saa za Afghanistan kwenye barabara ya mashariki mwa mji mkuu, inayoelekea katika mji mkubwa wa Jalalabad. Shirika la habari la REUTERS limebaini kwamba shambulizi hilo limnetokea katika kata ya Banae. Shambulizi hili lililengwa basi la lililokua limebeba wafanyakazi wa usalama kutoka Nepal. Raia wa Nepal wanatumiwa mara nyingi na ubalozi wa Marekani katika mji wa Kabul kwa ajili ya usalama wake.

Raia wa Nepal na wafanyakazi kutoka Afghanistan ni miongoni mwa wahanga, shirika la habari la REUTERS limeleza, likimnukuu mkuu wa polisi wa Kabul, Abdul Rahman Rahimi, aambalo limeongeza kuwa mshambuliaji alisubiri karibu na kampuni moja ambako walikuwa wakiishi wafanyakazi hao, na alifanya shambulizi hilo wakati gari lililokua likibeba wafanyakazi hao likifanya safari za asubuhi kuwapeleka kwenye maeneo ya kazi. Watu wengi ambao walikuwa katika soko jirani wamejeruhiwa.

Kwenye mitandao ya kijamii, msemaji wa wapiganaji wa kundi la Taliban, ambao walikua wakidai kuondoka kwa vikosi vya kigeni nchini Afghanistan, amekiri kuhusika na shambulio hilo, akibaini kwamba shambulizi hilo lilikua limelenga "vikosi vya uvamizi" nchini Afghanistan. "Mapema leo asubuhi tumeendesha shambulizi baya kabisa lililosababisha watu 20 kupoteza maisha," Zabihullah Mujahid amesema, na kuahidi kutoa "maelezo zaidi".

Haibatullah Akhundzada, kiongozi mpya wa Taliban

Hili ni shambulio la kwanza mjini Kabul tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Juni 6. Shambulio la mwisho lilitokea katika mji mkuu wa Afghanistan Aprili 19. Shambulio hili lililodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la Taliban, lilisababisha vifo vya watu 64 na zaidi ya 340 kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.