Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Hollande Mashariki ya Kati: nchi tatu na majukumu matatu tofauti

François Hollande almehitimisha ziara yake Mashariki ya Kati. Rais wa Ufaransa alikuwa Jumanne nchini Jordan, hatua yake ya tatu na ya mwisho ya ziara hii ambapo ametembelea pia Misri na Lebanon.

Rais Hollande (katikati) na waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian walikutana, Jumanne Aprili 19, 2016, na askari wa Ufaransakatika kambi ya kijeshi ya Prince Hassan, Jordan.
Rais Hollande (katikati) na waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian walikutana, Jumanne Aprili 19, 2016, na askari wa Ufaransakatika kambi ya kijeshi ya Prince Hassan, Jordan. STEPHANE DE SAKUTIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa alizungumza Jumanne mchana na Mfalme Abdullah II mjini Amman kabla ya kutembelea kambi ya kijeshi ya Prince Hassan ambako kunapatika ndege za kivita za Ufaransa.

Nchi tatu na majukumu matatu tofauti kwa rais wa Ufaransa katika ziara yake Mashariki ya Kati. Nchini Jordan, François Hollande alivaa vazi la kiongozi wa kivita. Alitembelea kambi ya kijeshi ya Prince Hassan, Kaskazini-Mashariki mwa mji wa Amman, ambapo ndege za kivita za Ufgaransa zilitumwa.

Rais Hollande alikaribisha shughuli inayoendeshwa kwa mafanikio dhidi ya ngome za kundi la Islamic State (IS) mwezi uliopita. Na kama alivyosema nchini Misri, anatiwa wasiwasi na mazingira ya usalama wa kikanda.

Hata hivyo, nchini Misri ziara hii ilijikita katika masuala ya uchumi. Akiambatana na matajiri wa Ufaransa, François Hollande amezengumzana mwenyeji wake Abdel Fattah al-Sissi kuhusu biashara na kuweza kusaini mikataba kadhaa.

Nchini Jordan, Rais Hollande amekaribisha wanajeshi wa Ufaransa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.