Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Watu zaidi ya 30 wauawa katika shambulizi la Taliban Kabul

Zaidi ya watu 30 wameuawa na Mamia kujeruhiwa baada ya kundi la Taliban kutekeleza shambulizi la bomu mjini Kabul nchini Afganistan.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika la kujitoa mhanga kwa gari katika mji wa Kabul Aprili 19.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika la kujitoa mhanga kwa gari katika mji wa Kabul Aprili 19. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Taliban limekiri kutekeleza shambulizi hilo katika mtaa uliokuwa na idadi kubwa ya watu.

Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema walisikia mlipuko mkubwa na baadaye wakaona moshi mwingi ukizuka katika eneo hilo.

Mkuu wa jeshi la Polisi katika mji wa Kabul Abdul Rahman Rahimi amesema mmoja wa washambuliaji alijilipua katika mkasa huo huku mwingine akikabiliana na maafisa wa usalama.

Maafisa wanasema zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa huku baadhi wakielezwa kuwa katika hali mbaya na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Wizara ya Mambo ya ndani inasema, hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo mwaka huu na zaidi ya Kilo 100 ya vilipuzi vilitumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.