Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-SHAMBULIZI

Afghanistan: watu 2 wauawa katika shambulio la Taliban Kabul

Raia wawili, ikiwa ni pamoja na mvulana mwenye umri wa miaka 12, wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa Ijumaa wiki hii mjini Kabul wakati wa shambulio la kujitoa mhanga lililodaiwa kutekelezwa na Taliban dhidi ya mgahawa unaomilikiwa na raia wa Afghanistan, maarufu kwa wageni.

Shambulio la kujitoa mhanga kwa gari ladaiwa kutekelezwa na Taliban, dhidi ya mgahawa unaojulikana kwa jina la "Le Jardin", Januari 1, 2016 mjini Kabul.
Shambulio la kujitoa mhanga kwa gari ladaiwa kutekelezwa na Taliban, dhidi ya mgahawa unaojulikana kwa jina la "Le Jardin", Januari 1, 2016 mjini Kabul. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linatokea zikisalia siku kumi kabla ya mkutano unaolenga kuzindua mazungumzo na wapiganaji.

Kundi la Taliban, ambalo limeongeza mashambulizi tangu majira ya joto, limeendelea na mashambulizi ya kujitoa mhanga dhidi ya majeshi au raia yeyote wa kigeni nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na migahawa, nyumba za kulala wageni au, askari 13,000 wa umoja wa Nchi za Kujihami za magharibi (NATO) waliopelekwa nchini humo.

Shambulio la kujitoa mhanga la Ijumaa wiki hii lilikua limelenga mgahawa unaojulikana kwa jina la "Le Jardin", linalojihusisha na mapishi ya chakula cha Ufaransa, ambalo linamilikiwa na raia wa Afghanistan. Mgahawa huo unapatikana katika wilaya ya Qala-e-Fatullah.

"Jioni ya leo (Ijumaa), kumeendeshwa shambulio dhidi ya mgahawa wa wavamizi wa kigeni", msemaji wa kawaida wa wapiganaji hao, Zabiullah Mujahid, amebaini kwenye Twitter. Msemaji wa polisi inayohusika na uchunguzi mjini Kabul, Fraidoun Obaidi na chanzo cha Magharibi wamelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba mgahawa unaojulikana kwa jina la "Le Jardin" ulikua umelengwa.

"Raia wawili wa Afghanistan wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa", Fraidoun Obaidi ameliambia shirika la habri la Ufaransa AFP. Katika tweet, shirika lisilo la kiserikali la Italia EMERGENCY, ambalo linamiliki hospitali katika eneo la kati la mji wa Kabul, amesema kuwa mmoja wa watu waliouawa ni mvulana mwenye umri wa miaka 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.