Pata taarifa kuu
IRAQ-HAIDAR

Waziri mkuu wa Iraq atembelea Ramadi

Masaa ishirini na nne baada ya jeshi la Iraq ya kuudhibiti mji mzima wa Ramadi kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS), Waziri mkuu Haidar al-Abadi alitembelea eneo hilo Jumanne hii. Ziara inayoashiria udhibiti wa mji huo.

Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi katika mji wa Ramadi, Aprili 29, 2015.
Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi katika mji wa Ramadi, Aprili 29, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Haidar al-Abadi mwenyewe alitangaza ziara yake katika mji wa Ramadi kwenye akaunti yake ya Twitter. Na yeye pia kama kiongozi wa serikali ya Iraq, aliyepandisha bendera ya Iraq katikati mwa mji uliokombolewa kutoka mikononi mwa kundi la IS Jumatatu wiki hii.

Akiwasili mjini Baghdad kwa helikopta, Waziri mkuu ametembelea katika maeneo muhimu ya Ramadi. Amekutana na askari ambao walikua wakijihusisha na kutegua mabomu katika maeneo yaliodhibitiwa kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kundi la Islamic State. Askari, mashujaa wa ushindi huo, wamepongezwa na serikali ya Iraq.

Kumejitokeza mgawanyiko katika makabila ya Kisuni

Na kusisitiza umuhimu wa vita hivi kwa viongozi wa Iraq, Haidar al-Abadi ametangaza siku ya likizo nchini kote siku ya Alhamisi.

Lakini ushindi bado bado unakabiliwa na hali ya sintofahamu. Vita bado vinaendelea katika baadhi ya maeneo ya mji wa Ramadi katika baadhi ya maeneo ya jiji. Bado kuna uhasama kati ya makabila ya Kisuni mjini Baghdad. Kuna baadi ya watu kutoka makabila hayo wanaoiunga mkono serikali ya Baghdad na wengine wanaendelea kuunga mkono kundi la Islamic State ambalo linasema bado linaendelea na harakati zake katika mji wa Ramadi. Makombora matatu yameanguka hata hivyo kwenye umbali wa mita 500 kutoka eneo ambapo Haidar al-Abadi alikua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.