Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-IRAN-USHIRIKIANO

Iran: Putin na Khamenei wathibitisha kumunga mkono Assad

Rais wa Urusi Vladimir Putin aliewasili mjini Tehran Jumatatu hii mchana, amekwenda moja kwa moja kukutana na Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ili kusisitiza "umoja wa maoni kati ya Moscow na Tehran" kuhusu Syria, akibainisha muungano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akikutana kwa mazungumzo na Kiongozi mkuu wa Iran Ali Khamenei, jijini TehranNovemba 23.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akikutana kwa mazungumzo na Kiongozi mkuu wa Iran Ali Khamenei, jijini TehranNovemba 23. AFP / HO / KHAMENEI.IR
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin na Ayatollah Ali Khamenei wamesisitiza umoja wao wa maoni kuhusu Syria, hali inayoonyesha kuwa hakukuwa na uhasama kati ya nchi hizo mbili ambazo ni wafuasi wa kuu wa Rais Bashar Al Assad.

Tehran na Moscow wanasaidia kifedha, kisiasa na kijeshi utawala wa Rais wa Syria na wameuongezea nguvu ushirikiano huo katika miezi ya karibuni. Urusi imeongeza zaidi mashambulizi yake dhidi ya makundi ya waasi nchini Syria, ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State. Tehran pia imeongeza uwepo wa washauri wake wa kijeshi na watu wakujitolea kijeshi katika uwanja wa vita.

Putin na Khamenei pia wamepinga shinikizo kutoka nje kwa kulazimisha mabadiliko ya utawala nchini Syria. Kauli hii inalenga Marekani, Ufaransa, lakini pia Saudi Arabia ambao wanalazimisha kuondoka kwa Rais Assad. Ayatollah Khamenei amesema kwa upande wake kuwa kuna haja ya kuharibu mipango ya Wamarekani ambao wanataka kutawala Syria na kudhibiti Ukanda wa Mashariki ya Kati. Hali hiyo ni tishio kwa Iran na Urusi, amesema Ayatollah Khamenei.

Ziara hii inaashiria uimarishaji wa muungano kati ya Tehran na Moscow katika ngazi ya kikanda na kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.