Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-HIJJA-USALAMA

Hijja: Iran yawatwisha mzigo wa lawama viongozi wa Saudia

Viongozi wa Iran wameelezea masikitiko yao kufuatia vifo vya mamia ya raia kutoka nchi hiyo waliofariki kufuatia mkanyagano katika mji wa Makkah Alhamisi wiki hii, na wengine wengi kujeruhiwa wakiwa katika ibada ya Hijja.

Mji wa Mina, karibu na mji mtakatifu wa Makkah, ambapo zaidi ya watu 700 wamefariki kufuatia mkanyagano wa Mahujaji Septemba 24, 2015.
Mji wa Mina, karibu na mji mtakatifu wa Makkah, ambapo zaidi ya watu 700 wamefariki kufuatia mkanyagano wa Mahujaji Septemba 24, 2015. REUTERS/Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya ajali ya Alhamisi Septemba 24 nchini Saudi Arabia. Pia amesema kuwa Saudi Arabia inapaswa kukubali kuhusika kwake katika tukio hilo. Afisa mwandamizi kwenye ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ameitishwa kwenye wizara ya mambo ya nje ya Iran, ili aweze kujieleze kuhusu tukio hilo, ambapo zaidi ya Mahujaji 700 wamefariki na wengine zaidi ya 800 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Tehran, Siavosh Ghazi, Iran tayari imesimamishwa miezi michache iliyopita Hijja ndogo katika mji mtakatifu wa Makkah kufuatia shambulio dhidi ya Mahujaji wawili kutoka Iran. Shambulio ambalo linaaminika kuwa, kwa mujibu wa viongozi wa Iran, lilitekelezwa na maafisa wa vyombo vya usalama katika uwanja wa ndege wa Saudi Arabia.

Wabunge na viongozi wa Iran pia wameshutumu kile walichokiita "uzembe" wa serikali ya Saudi Arabia kwa kuandaa Hijja, lakini pia kwa maandalizi ya msaada kwa majeruhi.

Uhusiano kati ya Iran yenye watu wengi kutoka dhebu la Shia na Saudi Arabia yenye watu wengi kutoka dhehebu la Sunni umedorora katika miaka ya hivi karibuni kutokana na hali inayojiri katika Ukanda huo vile vile na ushindani kati ya nchi hizi mbili. Tehran na Riyadhzinapingana kutokakana na hali inayojiri nchini Syria, Bahrain au Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.