Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: shambulio jipya karibu na uwanja wa ndege wa Kabul

Shambulio la kujitoa mhanga linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban limewaua watu watano na makumi wengine wamejeruhiwa karibu na uwanja wa ndege wa Kabul.

Askari wa polisi wa Afghanistan kwenye eneo la shambulio lililowaua watu wengi karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, Agosti 10 mwaka 2015.
Askari wa polisi wa Afghanistan kwenye eneo la shambulio lililowaua watu wengi karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, Agosti 10 mwaka 2015. REUTERS/Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea Jumatatu alaasiri wiki hii. Ni mfululizo wa mwisho wa mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu wengi katika mji mkuu wa Afghanistan tangu juma lililopita.

Shambulio hilo limetokea kwenye barabara yenye magari mengi ya uwanja wa ndege wa Kabul, barabara ambayo inatumiwa zaidi na vikosi vya usalama, amesema naibu mkuu wa polisi katika mji wa Kabul, Sayed Gul Agha Rouhani. Mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa (AFP) amejielekeza eneo la tukio na ameona mwoshi mkubwa ukifumba eneo lote la tukio, huku magari ya kusafirisha wagonjwa yakijielekeza kwenye hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni zilizotolewa asubuhi na viongozi wa serikali za mitaa, raia watano wameuawa na watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio hilo. "Mashambulizi ya kujitoa mhanga yalikuwa na lengo la kusababisha maafa makubwa miongoni mwa raia wa kawaida", msemaji wa polisi Kabul amehakikisha.

Afisa moja wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Kabul, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake, amesema kuwa safari za ndege zimesitishwa "kwa saa chache zijazo". Na Mamlaka ya usafiri wa Anga ya Pakistan imtangaza kuwa safari za ndege ziliokua zimepangwa kati ya Kabul na nchi jirani ya Pakistan zimesitishwa kutokana na shambulio hilo.

Kundi la Taliban lakiri kuhusika na shambulizi

Msemaji wa kawada wa kundi la Taliban, Zabihulla Mujahid amekiri mbele ya shirika la habari la Ufaransa kuwa Taliban ndio imeendesha shambulio hilo. Kwa mujibu wa shirika hilo, msemaji wa kawaida wa Taliban ametangaza kuwa shambulio hilo limekua limelenga "magari mawili ya vikosi vya wanajeshi wa kigeni".

Wanajeshi wa NATO, lakini pia na hasa polisi na jeshi vya Afghanistan, vimekua vilengwa na mashambulizi ya waasi wa kiislam tangu kuanguka kwa utawala wao mwaka 2001, ingawa raia ndio waathirika wa kwanza katika machafuko hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), raia 1,592 wameuawa na wengine 3,329 wamejeruhiwa katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu katika ongezeko la machafuko.

Wimbi la mashambulizi yasababisa maafa

Kundi la Taliban limenyooshewa kidole kwamba lilitekeleza mashambulizi mengine mawili yaliosababisha vifo vingi katika mji wa Kabul, ikiwa ni pamoja na watu 27 waliouawa mbele ya chuo cha polisi Ijumaa Agosti 7. Ni mawimbi ya kwamza ya mashambulizi tangu uteuzi wa Akhtar Mansour kwenye uongozi wa kundi la waasi zaidi ya siku kumi na tano zilizopita, akichukua nafasi ya Mullah Omar, kiongozi wa kiroho wa Taliban, ambaye kifo chake kilitangazwa mwishoni mwa mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.