Pata taarifa kuu
THAILAND-MALAYSIA-BURMA-UHAMIAJI

Thailand: mkutano wa kikanda kuhusu uhamiaji

Zaidi ya mataifa kumi na tano yatawakilishwa Ijumaa wiki hii katika mkutano wa kikanda utakaofanyika katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, baada ya boti kadhaa ziliyokua zikisafirisha wahamiaji kuokolewa majuma ya hivi karibuni.

Wahamiaji kutoka jamii ya Rohingyas wakiwasili Acheh, Indonesia, Mei 27 mwaka 2015.
Wahamiaji kutoka jamii ya Rohingyas wakiwasili Acheh, Indonesia, Mei 27 mwaka 2015. REUTERS/Darren Whiteside
Matangazo ya kibiashara

Wanaume, wanawake na watoto, wengi wao wakitokea nchini Burma na Bangladesh waliokolewa katika boto hizo wakikimbia nchi zao kutoakana na mateso na umaskini. Hali hiyo imesababisha vifo vya watu kadhaa, huku suluhu kwa matatizo hayo linaweza kupatiwa jawabu kiukanda na kisiasa.

Si mara ya kwanza kwa nchi za ukanda huu kujaribu kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na utitiri wa wahamiaji, lakini wakati huu mkutano huo umeitishwa kidharura kulingana na hali ya wahamiaji ambayo imekithiri katika baadhi ya nchi za ukanda huu.

Kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Burma hatimaye limesema litaitikia mwaliko huo wa Bangkok. Hata hivyo kundi hili limetishia kuondoka kwenye meza ya mazungumzo kama suala la Rohingyas litazungumziwa. Katika mkutano huo zinatazamiwa kushiriki nchi za Malaysia, Indonesia pamoja na Thailand ambayo inaathirika zaidi na utitiri wa wahamiaji wiki za hivi karibuni.

Vita dhidi ya wafanyabiashara haramu

Kwa jumla ya wahamiaji 25,000 walitoroka nchi zao wakipitia baharini katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2015, gazeti la New York Times limekumbusha. Moja ya sababu zake zimetajwa kwa mara ya kwanza. Katika mkutano wa Bangkok suala la vita dhidi ya walanguzi na wafanyabiashara haramu litapewa kipaumbele, baada ya miaka ya kutokuchukua hatua au njama za baadhi ya viongozi. Kwa sababu kuodoka kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu inaonekana kuwa ni jambo ambalo limeandaliwa kwa upana na kundi la watu katika nchini mbalimbali za ukanda huu tangu mwanzoni mwa msafara katika nchi za Burma na Bangladesh, lakini pia katika nchi wanakofikia na nchi wanakopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.