Pata taarifa kuu
JORDAN-IS-HAKI ZA BINADAMU

Mfalme Abdallah aapa kuendelea na vita dhidi ya IS

Mfalme wa Jordan wa Abdallah wa pili, anasema atatumia mbinu zote kuliangamiza kundi la Islamic State baada ya kundi hilo kumuua kwa kumteketeza moto Rubani Moaz al-Kasasbeh.

Raia wa Jordan wakija kumlaki Mfalme Abdallah II akirejea nchini akitokea Marekani, Februari 4 mwaka 2015.
Raia wa Jordan wakija kumlaki Mfalme Abdallah II akirejea nchini akitokea Marekani, Februari 4 mwaka 2015. REUTERS/Majed Jaber
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya mfalme Abdullah imekuja baada ya kurejea nchini kutoka Marekani na kuongoza kikao cha dharura cha usalama jijini Amman.

Baada ya kuuawa kwa rubani huyo, Jordan iliamua kulipiza kisasi kwa kuwauawa kwa kuwanyonga raia wawili wa Iraq ambao wamekuwa wakishikiliwa kwa makosa ya ugaidi.

Siku Jumatano iligubikwa na sala au kusalia kimya kwa muda wa dakika kadhaa kwa kutoa heshima kwa Moaz Kasasbeh. Vyama vya upinzani na vile vinavyounga mkono utawala ulioko madarakani, vimelaani kwa pamoja mauaji ya kikatili ya rubani huyo wa Jordan.

Alipowasili katika mji mkuu wa Jordan, Amman, mbele ya maafisa wake, Mfalme Abdallah II, alisema kwamba Jordan itaendelea kushiriki katika vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislam kwa kutetea Uislamu na maadili ya Jordan.

Lakini mbele ya Wabunge kadhaa wa Bunge la Marekani Congress Mfalme Abdallah II, alisema kwamba kitu pekee kitakacho sababisha Jordan inajiondoa katika vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislam ni kukosa silaha na mafuta. Kwa upande wa Washington inaonekana wazi kwamba Jordan bado inasalia katika muungano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.