Pata taarifa kuu
JORDAN-IS-HAKI ZA BINADAMU

Jordan imewanyonga wanamgambo wa IS

Serikali ya Jordan imesema imewaua kwa kuwanyonga wanajihadi wawili raia wa Iraq ambao ni washirika wa karibu wa kundi la Kiislamu la Islamic State.

Baada ya kutangazwa kuuawa kwa rubani wa Jordan, raia wa Jordan wamepandwa na hasira. Baadhi walijielekeza katika nyumba wanakotolea salaamu za rambirambi kwa watu waliofariki kutoka kabila la Moaz Kasasbeh, mjini Amman.
Baada ya kutangazwa kuuawa kwa rubani wa Jordan, raia wa Jordan wamepandwa na hasira. Baadhi walijielekeza katika nyumba wanakotolea salaamu za rambirambi kwa watu waliofariki kutoka kabila la Moaz Kasasbeh, mjini Amman. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wamekua wakizuiliwa jela nchini Jordan, kwa tuhuma za kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu

Hatua hii imechukuliwa baada ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kumuua kwa kumchoma moto rubani wa Jordan Maaz al-Kassasbeh waliyekuwa wanamshikilia.

Msemaji wa serikali ya Jordan amethibitisha kunyongwa kwa wawili hao ambao ni mlipuaji wa kujitoa mhaga Bi Sajida al-Rishawi na Ziad al-Karboli.

Kitendo cha kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kuumua kwa kumchoma moto rubani wa Jordan kimelaaniwa Kimataifa, na kumlazimu Mfalme Abdullah aliyekuwa ziarani nchini Marekani kusitisha ziara hiyo.

Rais Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliolaani mauji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.