Pata taarifa kuu
JORDAN-IS-SYRIA-UGAIDI-USALAMA

Ndege ya Jordan yaanguka, rubani mikononi mwa IS

Rubani wa ndege ya kijeshi ya Jordan yuko mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Syeria.

Rubani wa jeshi la anga la Jordan aliye pigwa picha Mei 12 mwaka 2014 wakati ndege yake ilipokua ikipaa hewani.
Rubani wa jeshi la anga la Jordan aliye pigwa picha Mei 12 mwaka 2014 wakati ndege yake ilipokua ikipaa hewani. AFP PHOTO HANDOUT-US AIR FORCE / SSGT Brigitte N. Brantley
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Jordan limethibitisha kwamba ndege aliyokua akiendesha rubani huyo imeanguka Jumatano Desemba 24 katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kundi hilo katika jimbo la Raqqa, kaskazini mwa Syria.

Picha ambazo zimekua zikiwekwa hewani kwenye mitandawo tofauti duniani zinaonesha mtu akivalia T-shirt nyeupe, huku akizungukwa na wapiganaji wenye silaha. Picha zingine zimekua zikionyesha mabaki ya ndege ambayo inadaiwa kuwa ni mabaki ya ndege ya Jordan, ambayo haikurejea leo Jumatano Desemba 24 baada ya kutekeleza wajibu wake katika anga ya Syria katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Jordan ni moja ya nchi za kiarabu ziliyokubali kushiriki katika operesheni ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Saudia Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrein na Qatar ni miongoni mwa nchi hizo za kiarabu zinazoshiriki katika operesheni hiyo. Majeshi ya nchi hizo yanaendesha mara kwa mara operesheni hiyo nchini Iraq na Syria, ambapo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam wanaendesha harakati zake.

Ni katika operesheni hiyo iliyokua ikiendeshwa katika jimbo la Raqqa, ambapo ndege hiyo ilipoanguka. Hata hivyo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limekiri kuidungua ndege hiyo kwa kombora, licha ya kuwa Jordan imeendelea kusisitiza kuwa ndege yake hiyo ilianguka katika mazingira ya kawaida.

Shirika la haki za binadamu la Syria limethibitisha kuwa ndege hiyo ya Jordan imedunguliwa kwa kombora. Eliot Higgins, mtaalamu wa masuala ya silaha, ambaye amenukiuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, amebaini kwamba kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam linamiliki makombora yanayotumiwa kwa kudungua ndege ambayo yalitengenezwa nchini China na Urusi.

Ni kwa mara ya kwanza mwanajeshi wa vikosi vya muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kukamatwa na wapiganaji wa kundi hilo. Baba wa rubani huyo wa Jordan ametolea wito kundi la wapiganaji wa Dola la kiislam “kumsamehe” mwanaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.