Pata taarifa kuu
GAMBIA-TAIWANI

Nchi ya Gambia yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na taifa la Taiwani

Serikali ya Gambia imetangaza kuvunja uhusiano wake wa kibalozi na nchi ya Taiwan baada ya kushirikiana kwa zaidi ya miaka 18, katika kile nchi hiyo imedai kuwa ni kwasabababu za kimaslahi.Tangazo la rais Yahya Jammeh linaifanya nchi ya Gambia kuwa taifa la kwanza barani Afrika kukatisha uhusiano wa kibalozi na taifa la Taiwan toka kuingia madarakani kwa rais Ma Ying-Jeou mwaka 2008.Β 

Rais wa Taiwan akiwa na mwenyeji wake rais Gambia, Yahya Jammeh hivi karibuni
Rais wa Taiwan akiwa na mwenyeji wake rais Gambia, Yahya Jammeh hivi karibuni Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake, rais Jammeh amesema kuwa uamuzi wa kuvunja uhusiano wa kibalozi na taifa hilo unatokana na sababu za kmaslahi na kusisitiza kuwa licha ya kusitisha uhusiano huo, nchi yake bado itaendele akushirikiana na wananchi wa Taiwan.

Nchi ya Gambia pia ilikuwa ni taifa la kwanza kuendelea kuwa na uhisiano na taifa la Taiwan hata baada ya utawala wa China kuanza operesheni ya ushirikiano na mataifa ya Afrika kwa kutangaza msaada wa mabilioni ya fedha kwa nchi hizo.

Waziri wa mambo ya nje wa Taiwan, Simon Ko akizungumza na wanahabari mjini Taipei, ameeleza kushtushwa kwake na hatua ya Gambia kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi yake na kwamba itaendelea kutambuliwa na mataifa 22 duniani hasa ya nchi zinazoendelea.

Serikali ya Beijing inaitambua nchi ya Taiwan kama sehemu ya taifa lake baada ya nchi hiyo kujitenga na China mwaka 1949 baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenye jambo ambalo sasa ni wazi linadhihirisha kuwepo kwa hali ya sintofahamu kayi ya mataifa haya mawili.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya Gambia kutangaza kuacha uhusiano na nchi ya Taiwan imetokana na ushawishi wa Serikali ya Beijing ambayo siku za hivi karibuni imekuwa ikiyashawishi baadhi ya mataifa kutoshirikiana na nchi ya Taiwan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.