Pata taarifa kuu
HEZBOLLAH-SYRIA

Kiongozi wa kundi la Hezbollah asisitiza wapiganaji wake kusalia nchini Syria

Kiongozi wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon ambalo wapiganaji wake wanapigana samabana na jeshi la Syria, amesema wapiganaji wake wataendelea kuisaidia Serikali ya nchi hiyo mpaka pale vita hivyo vitakapomalizika. 

Kiongozi wa kundi la Hezbollah, Hassan Nasrallah
Kiongozi wa kundi la Hezbollah, Hassan Nasrallah REUTERS/Khalil Hassan
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na maelfu ya waumini wa madhehebu ya Kishia wakati wa Sherehe za Shura, kiongozi wa Hezbollah, Haasan Nasrallah amewahakikishia wafuasi wake kuwa jeshi lake litaendelea kuusaidia utawala wa Damascus dhidi ya makundi ya kigaidi.

Wanamgambo wa Hezbollah wametoa mchango mkubwa kwa jeshi la Syria ambapo wamefanikiwa kuurejesha mji wa Qusair na maeneo ya Damascus kwenye himaya ya Serikali na sasa wameanza operesheni maalumu kuelekea mji wa Aleppo na maeneo mengine.

Haasan amekosoa juhudi ambazo zinafanya na mataifa ya magharibi kwa kushirikiana na nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Kiarabu katika kujaribu kuuangusha utawala halali wa rais Bashar al-Asad.

Kundi hilo litajwa na utawala wa Marekani kama sehemu ya makundi ya kigaidi duniani hasa baada ya kutangaza kuingia kwenye ardhi ya Syria kupigana mstari wa mbele na wanajeshi wa serikali katika kukabiliana na waasi wa jeshi huru la Syria.

Kwa mara ya kwanza akizungumza hadharani toka mafichoni kusini mwa mji wa Beirut, Hassan Nasrallah anasema kuwa wapiganaji wake wanapigania haki ya wananchi wachache wa Syria ambao wananyanyasika kutokaa na uasi unaendelea kufanywa na makundi ya kigaidi nchini humo.

Haya yanajiri wakati huu ambapo nchi ya Korea Kaskazini imekanusha vikali taarifa kuwa inausaidia kwa silaha utawala wa Syria.

Hivi karibuni gazeti moja nchini Israel liliandika habari kuwa kuna marubani wa ndege za kivita ambao wako nchini Syria kuusaidia utawala wa rais Asad, tuhuma ambazo utawala wa Korea Kaskazini unakanusha vikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.