Pata taarifa kuu
UFILIPINO-VIETNAM-TYPHOONE HAIYAN

Kimbunga cha Typhoon Haiyan chaelekea nchini Vietnam, madhara yaanza kushuhudiwa

Kimbunga cha Typhoon Haiyan kimeshuhudiwa kwenye nchi ya Vietnam mapema leo asubuhi ambapo miti na milingoti ya umeme na mapaa ya baadhi ya nyumba yameezuliwa kutokana na upepo mkali, saa chache baada ya kimbunga hicho kuleta madhara makubwa nchini Ufilipino. 

Moja ya miji nchini Ufilipino ambayo ilikumbwa na kimbunga cha Typhoon Haiyan
Moja ya miji nchini Ufilipino ambayo ilikumbwa na kimbunga cha Typhoon Haiyan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Vietnam imeanza shughuli za kuwahamisha maelfu ya wananchi wake wanaoishi kwenye maeneo ya pwani ambako kimbunga hicho kimeelekea na kuagiza wanajeshi kuharakisha usafiri wa kuwahamisha watu hao.

Leo asubuhi tayari kimbunga hicho kimeanza kuleta madhara kwenye baadhi ya maeneo ambapo kumeripotiwa kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba na kung'olewa kwa miti mikubwa.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imeonya watu wanaoishi kwenye maeneo ya pwani na maeneo ambayo kimbunga hicho kinatarajiwa na kutaka wahame kwa muda kwa hiari yao kabla ya madhara zaidi.

Kimbunga hivyo kimeelekea nchini Vietnam saa chache baada ya kuleta madhara makubwa nchini Ufilipino ambapo watu zaidi la laki moja wanakadiriwa kupoteza maisha kutokana na kimbunga hicho.

Watu zaidi ya laki 6 na elfu 50 wamehamishwa mwishoni mwa juma nchini Vietnam kuhofia madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na mvua zinazoambatana na upepo mkali.

Vikosi vya uokoaji nchini Ufilipino vinaendelea na juhudu za kuwasaka manusura wa kimbunga hicho licha ya kukiri kuwa kuna matumaini madogo ya kuwapata watu wengine wakiwa hao.

Bado hasara rasmi iliyotokana na kimbunga hicho haijatangazwa na Serikali licha ya kudai kuwa itahakikisha wananchi wake wote walioathirika na kimbunga hicho wanapatiwa msaada wa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.