Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BRICS

Nchi wanachama za BRICS zakubaliana kuanzisha benki yao ya maendeleo

Mataifa ambayo uchumi wake unakuwa kwa haraka duniani yanayotambulika kama BRICS yanayozijumuisha nchi ya Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini yamefikia makubaliano ya kuanzisha Benki ya Maendeleo ambayo itashindana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha Duniani IMF. 

Viongozi wanaounda muungano wa kiuchumi wa BRICS wakiwa kwenye picha ya pamoja mjini Durban, Afrika Kusini wanakoendelea na mkutano wao
Viongozi wanaounda muungano wa kiuchumi wa BRICS wakiwa kwenye picha ya pamoja mjini Durban, Afrika Kusini wanakoendelea na mkutano wao REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Mawaziri wa Fedha kukutana hiyo jana Jijini Durban ambapo wameafikiana kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kupiga hatua kwa kasi zaidi.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Pravin Gordhan baada ya kufikiwa makubaliano hayo akazungumza na wanahabari na kuwaeleza lengo la nchi hizo tano ni kuhakikisha uchumi wao unaimarika zaidi na kujiepusha na kudorora kwa uchumi.

Viongozi wa muungano huo wametagaza kufikia mpango huo kutokana na kushindwa kwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF katika kushughulikia matatizo sugu ya ukuaji wa uchumi kwenye mataifa mengi ya dunia.

Benki ya Dunia yenyewe kwa upande wake ilitangaza kuwa tayari kushirikiana na nchi wanachama za BRICK katika kuhakikisha zinafanikisha kufunguliwa kwa benki hiyo ya maendeleo ambayo italenga kuzisaidia nchi wanachama.

Mbali na kujadili kuwa na taasisi moja ya fedha nchi hizo pia zimepongeza uhusiano uliopo kati ya mataifa ya Afrika na nchi ya China ambayo imewekeza pakubwa barani humu na kwamba wataendelea kushirikiana nayo licha ya ukosolewaji toka mataifa ya magharibi.

Katika kuonesha kuwa zipo tayari kushirikiana na China, nchi ya Brazil hapo jana zilitiliana saini mikataba ya kimaendeleo katika sekta ya mafuta ambayo itashuhudia nchi hizo mbili zikinufaika na biashara.

Katika hatua nyingine nchi wanachama pia zimependekeza kuboreshwa kwa bandari zilizoko kwenye nchi wanachama ili kuhakikisha zinakabiliana na mdororo wa kiuchumi ambao mara baada ya kuyakumba mataifa ya Ulaya hata bandari za nchi wanachama zilipunguza utendaji kazi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.