Pata taarifa kuu
MALI

Waziri Mkuu wa Mali Cheik Modibo Diarra ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Mali Cheik Modibo Diarra amejiuzulu saa chache baada ya kukamatwa na wanajeshi waliopindua serikali hiyo mapema mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Diarra alikamatwa siku ya Jumatatu nyumbani kwake jijini Bamako baada ya agizo kutoka kwa kiongozi wa kijeshi aliyeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi Amadou Sanogo.

Jumuiya ya Kimataifa ikiongozwa na Ufaransa imeshtumu kitendo cha wanajeshi kumlazimisha Diarra kuachia madaraka, huku Umoja wa Ulaya ukitaka Waziri Mkuu mpya kuteuliwa haraka iwezekanavyo na wanajeshi kuacha kujiingiza katika maswala ya siasa.

Duru zinasema kuwa hueda Diarra akasafiri Ufaransa kwa hifadhi kwa hofu ya usalama wake, na wakati akitangaza kujiuzulu yeye pamoja na serikali yake hakutoa sababu maalum ya kuchukua uamuzi huo.

Diarra aliteuliwa mwezi Aprili baada ya jeshi kukabidhi madaraka kwa umma ili kuundwa kwa serikali ya mpito baada ya shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa na Umoja wa Afrika.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Diarra na wale waliopindua serikali ya Mali chini ya kiongozi wao Sanogo.

Wakati wa uongozi wake kama Waziri Mkuu, Diarra alikuwa tayari na viongozi wengine wa matafa ya Arika Magharibi kutuma majeshi ya ECOWAS Kaskazini mwa Mali kukabiliana na makudi ya waasi yanayotawala eneo hilo.

Idadi kubwa ya wanajeshi wa  Mali wanapinga wazo la kepelekwa kwa wanajeshi wa Kimataifa Kaskazini mwa nchi hiyo kwa kile wanachokisema kuwa wao wanaweza kupambana na makundi hayo  ikiwa watapata msaada wa kifedha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.