Pata taarifa kuu
RWANDA-UGANDA-USHIRIKIANO

Kagame na Museveni kukutana tena chini ya upatanishi wa Lourenço na Tshisekedi

Marais wa Uganda na Rwanda wanatarajia kukutana tena Ijumaa hii Februari 21 katika mpaka wa Uganda na Rwanda wa Katuna katika juhudi za kuendeleza mchakato wa kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, ambao ulikuwa unalega lega.

Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusainiwa makubaliano ya kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili jirani, Jumatano Agosti 21, 2019.
Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusainiwa makubaliano ya kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili jirani, Jumatano Agosti 21, 2019. JOAO DE FATIMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia wa pande zote mbili wanatarajia marais hao watafungua mpaka wa Gatuna uliofungwa mwezi wa Februari mwaka jana na kurudisisha uhusiano mwema wa mataifa hayo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake Yoweri Museveni wa Uganda wamekuwa wakikutana na kuafikiana kuhusu kuimarisha uhusiano kati yao ili kumaliza uhasama uliopo.

Wiki hii Serikali ya Uganda iliwaachia huru raia wengine 13 wa Rwanda waliokuwa wamezuiliwa katika jela zake wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Kwa mjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa, raia hao wa Rwanda ni wale waliokamatwa mwaka 2019 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kukutwa na silaha.

Hili ni kundi la pili baada ya Wanyarwanda wengine kukabidhiwa mapema mwezi wa Januari mwaka 2020, katika hatua ya kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo.

Rwanda imekuwa ikishtumu Uganda kuwapa hifadhi waasi wanaotaka kuhatarisha usalama wake, ikuwafunga kiholela raia wake, huku Uganda ikiishtumu Rwanda kuandaa kundi la watu ili kuhatarisha usalama wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.