Pata taarifa kuu
RWANDA-SANAA-SIASA-USALAMA

Rwanda: Mwimbaji wa injili Kizito Mihigo apatikana amefariki dunia gerezani

Polisi ya Rwanda imetangaza kifo cha mwimbaji wa injili Kizito Mihigo ambaye amepatikana amefariki dunia gerezani baada ya kujiua, mamlaka imesema.

Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa.
Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja na nusu baada ya kuachiliwa huru kwa msamaha wa rais, Kizito Mihigo alikamatwa tena Februari 13, 2020. Alikuwa anashtakiwa makosa yanayaohusiana na jaribio la kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter leo Jumatatu Februari 17, polisi ya Rwanda imebaini kwamba mwimbaji Kizito Mihigo alikutwa amefariki duniakatika chumba chake alipokuwa anazuiliwa mwendo wa saa 11:00 alfajiri. Mamlaka imesema kuwa mwimbaji huyo alijiua, bila kutoa maelezo zaidi, na kuongeza kwamba imeanzisha uchunguzi.

Mwimbaji huyo wa injili alikuwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Remera katika mji mkuu Kigali kwa siku tatu. Alikamatwa Februari 13 katika wilaya ya Nyaruguru, Kusini Mashariki mwa Rwanda. Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) ilikuwa inashtumu makosa yanayaohusiana na jaribio la kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha, na kwa kujaribu kutoa hongo kwa wanakijiji ambao walimwona.

Tangu wakati wa kukamatwa kwake, ndugu zake walielezea mshangao wao kusikia habari hizo za kutaka kuvuka mpaka kuingia nchini Burundi, na kuhakikisha kwamba hakuwa amewaambia kuhusu mpango wa kuondoka nchini Rwanda.

Kizito Mihigo ambaye hapo awali aliokekana kama mtetezi wa maridhiano na mmoja wa waimbaji mashuhuri nchini Rwanda, alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014. Wakati huo alikuwa alitoweka kwa siku kadhaa kabla ya mamlaka kuthibitisha kukamatwa kwake.

Kizito Mihigo, ambaye alikuwa mmoja wa manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, alifungwa jela kwa kipindi cha miaka minne, akishutumiwa makosa yanayohusiana na kula njama dhidi ya kuhatarisha usalama dhidi ya Rwanda. Mwishowe aliachiliwa huru mwezi Septemba 2018 kwa uamuzi wa rais Paul Kagame, pamoja na mpinzani wa kisiasa, Victoire Ingabire.

Kizito Mihigo alipata umaarufu kutokana na nyimbo zake kama vile 'Inuma' unaomaanisha njiwa na 'Turi abana b'u Rwanda'ukimaanidha tuko watoto wa Rwanda.

Hii hapa ni moja ya nyimbo alizoimba unaitwa 'Turi abana b'u Rwanda'

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.