Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-UGANDA-MAZINGIRA-ZIWA-VICTORIA

Shughuli za Kibinadamu zinachangia Uchafuzi wa Maji ya Ziwa Victoria

Shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji ya Ziwa victoria katika nchi zinazolizunguka ziwa hilo kumechangia kuongezeka kwa uchafuzi wa maji, hali inayosababisha kupungua kwa idadi ya Samaki na viumbe hai wengine wanaopatikana katika ziwa hilo.

FILE PHOTO: Men on camels cross the water as a woman washes clothes in Lake Chad in Ngouboua, January 19, 2015. REUTERS/Emmanuel Braun/File Photo
FILE PHOTO: Men on camels cross the water as a woman washes clothes in Lake Chad in Ngouboua, January 19, 2015. REUTERS/Emmanuel Braun/File Photo REUTERS/Emmanuel Braun/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Uganda ,Kenya na Tanzania ni wanufaika wa moja kwa moja wa ziwa hilo, lakini suala la uchafuzi katika vyanzo vya maji yanayoingia katika ziwa hilo ni changamoto, Florence H. Mahay Mkurugenzi wa Bodi ya maji ya ziwa hilo anasema wamefanya jitihada za kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuunda kamati maalum za zinazohusisha wananchi.

Mbali na Uchafuzi huo, Shughuli za kibianadamu nazo zimeonekana kuathiri viumbe hai vilivyomo katika ziwa hilo ikiwa ni pamoja na samaki, Watafiti wanasemaje? Ishmael Timirey ni Mkurugenzi wa Bodi ya maji ziwa Victoria.

Akizungumzia hali ilivyo kwa sasa Mtafiti wa Ekolojia ya maji baridi na Mdhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Dakta Lulu Kaaya anasema hali ni mbaya kutokana na kemikali, mabadiliko ya tabia nchi kuathiri samaki na viumbe wengine waliomo katika ziwa hilo.

Serikali ya Ufaransa imechukua hatua mbalimbali kusaidia wakulima kuondokana na matumizi ya kemikali katika kilimo ili maji yanayoingia katika ziwa kutoka kathiri viumbe waliomo, Frederic Clavier Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ansema serikali yake

      Nimeamua kwa jina la ufaransa kutoa kutoa Dola milioni moja za kimarekani kwa Tanzania, Agro ecology maana yake maana yake kupunguza matumizi ya kemikali, bidhaa za kemikali kwa wakulima- alisema Clavier

Utafiti uliofanyika miaka mitatui iliyopita ulionyesha kuwa robo tatu ya aina zote za viumbe hai waishio kwenye maji yasiyo ya chumvi katika Ziwa Victoria lililopo Afrika Mashariki wamo hatarini ya kuangamia kutokana na uchafuzi wa mazingira na uvuvi uliopindukia, Hali hiyo inahatarisha maisha ya takriban watu milioni 42 wanaoishi katika nchi za Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.