Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Mzozo wa mipaka na idadi ya majimbo vyaiweka Sudan Kusini njia panda

Makamu wa rais wa Afrika Kusini David Mabuza ambaye kwa sasa anaongoza juhudi za usuluhishi wa masuala tata nchini Sudan Kusini kuelekea uundwaji wa seirikali ya pamoja mwezi ujao, amependekeza kuahirishwa kwa upatikanaji wa suluhu kuhusu mzozo wa mipaka na idadi ya majimbo.

Salva Kiir na Riek Machar Septemba 12, 2018.
Salva Kiir na Riek Machar Septemba 12, 2018. YONAS TADESSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo na rais Salva Kiir, Mabuza amesema imekubaliwa kuwa suluhu ya mzozo huo ipatikane, baada ya siku 90 pindi tu serikali ya pamoja itakapoundwa.

Suala la mipaka na idadi ya majimbo limesalia tata, kati ya rais Kiir na mpinzani wake Riek Machar katika mchakato wa undwaji wa serikali hiyo.

Awali Salva Kiir alisema kuwa ikiwa suala la idadi ya majimbo litakuwa halijapatiwa ufumbuzi hadi wakati wa uundwaji wa serikali, serikali hiyo mpya ndio itahusika na kutafutia ufumbuzi swala hilo, pamoja na maswala mengine ambayo yatakuwa bado hayajapatiwa ufumbuzi.

Hivi karibuni rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar walijikubalisha kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari mwaka huu, baada ya kumalizika kwa siku 100 waliyopewa na viongozi wa ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.