Pata taarifa kuu
KENYA-AL SHABAB-ELIMU-USALAMA

Walimu wanaofunza Kaskazini Mashariki mwa Kenya wahofia usalama wao

Walimu nchini Kenya wanaofunza eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo wanaendelea kuhofia usalama wao, baada ya washukiwa wa Al Shabab kuwashambulia na kuwauwa wenzao wanne mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kaunti ya Garissa.

Nchini Kenya, katika mji wa Lamu, Al Shabab iliendesha shambulio na wasafiri walilindiwa usalama katika kambi ya jeshi, Januari 05, 2020.
Nchini Kenya, katika mji wa Lamu, Al Shabab iliendesha shambulio na wasafiri walilindiwa usalama katika kambi ya jeshi, Januari 05, 2020. © REUTERS/Abdalla Barghash
Matangazo ya kibiashara

Chama cha kutetea maslahi ya Walimu nchini humo KNUT sasa kinataka hatua za dharura na za makusudi kuchukuliwa na serikali ili kuwahakikishia usalama wa walimu hao.

Shambulizi katika shule ya Kamuthe, limezua hasira na wasiwasi miongoni mwa Walimu katika eneo hilo linalopakana na nchi ya Somalia.

Robert Kivuti mfanyikazi katika shule hiyo, alifanikiwa kujificha baada ya kutokea kwa shambulizi hilo, na kuimbia RFI, kuwa anahofia usalama wake.

“Serikali lazima imefanye jambo ili kutulinda. Ukweli, kuendelea kufunza katika mazingira haya, inakuwa ngumu,” alisema.

Katibu Mkuu wa chama cha Walimu nchini humo KNUT, Wilson Sossion anaitaka serikali kuwahakikishia usalama Walimu hao la sivyo watachukua hatua.

“Haitoshi tu kusema pole na kutuma risala za rambirambi. Serikali ihakikishe kuwa, walimu wetu wanakuwa salama. Hatuwezi kuendelea kuwa darasani, “ alisema Sossion.

Sossion anaona kupata tatizo la suala hili, wanafunzi wanaomaliza Sekondari katika eneo hilo lenye idadi kubwa ya Waislamu wenye asili ya Somalia, waruhusiwe kufunza katika shule hizo za serikali, kwa sababu Al Shabab imekuwa ikiwalenga wageni.

“Wanafunzi wanaomaliza Shule za sekondari wanaweza kupewa mafunzo ili wafunze katika maeneo yao, hili litasaidia kumaliza tatizo hili,” ameongeza Sossion.

Utafiti unaonesha kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, asilimia sabini ya Walimu, Madaktari na wafanyikazi wengine ambao sio wenyenji wa eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo wamecha kazi zao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.