Pata taarifa kuu
TEKNOLOJIA-BIOANUAI-WANYAMA-MAZINGIRA

COSTECH na DIT Kushirikiana Kuhifadhi Takwimu za Wanyama na Mazingira Tanzania

Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania (COSTECH) ikishirikiana na Taasisi ya Teknolojia Tanzania (DIT) wamesaini mkataba wa kuratibu namna bora ya kuhifadhi, kuchapisha na kutumia takwimu zinazuhusiana na baioanuai katika mazingira na wanyama nchini humo.

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),anayeshughulikia Utawala na Fedha, Dakta Najat Mohamed anayezungumza  jijini Dar es Salaam . kushoto ni Mkurugenzi wa COSTECH Dakta Amos Nungu.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),anayeshughulikia Utawala na Fedha, Dakta Najat Mohamed anayezungumza jijini Dar es Salaam . kushoto ni Mkurugenzi wa COSTECH Dakta Amos Nungu. Picha;COSTECH
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dakta Amos Nungu amesema, lengo ni kutafiti, na kutoa elimu pamoja na kuendeleza sekta baioanuai inahusisha mgawanyiko wa maisha ya wanyama na mazingira,ni muhimu taarifa kuhifadhiwa na tafiti ziweze kufanywa ambazo zitaelimisha kizazi hiki na kizazi kijacho

"Tunamradi wa pamoja kati ya DIT na COSTECH, lakini sisi ni waratibu, wadau wa mradi huo ni taasisi mbalimbali kulingana na majukumu yetu, tunaongelea mazingira na utalii nchini, sasa jitihada zichukuliwe ili kuhifadhi, kutunza, na kufanya tafiti ambazo zinaelimisha, sisi tuliopo na vizazi vijavyo"-Alisema Dakta Nungu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),anayeshughulikia Utawala na Fedha, Dakta Najat Mohamed amesema DIT ina jukumu la kuandaa mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za baioanuai, kwa kuwezesha kuapata taarifa za viumbe hai mbalimbali pamoja na Mazingira.

        "Taarifa za baioanuai ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote, maana bila viumbe hai hakuna maisha, bila mimea, wanyama na wadudu maisha ya binadamu yatakuwa hatalini maana ndio vyanzo vya chakula, hali ya hewa nzuri, mvua na mahitaji mengine ya binadamu kama dawa"-Alisema Dakta Najat

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa taarifa za, baianuai Tanzania amabe pia ni Mhadhiri chuo kikuu cha Kilimo SUA Kutoka Idara ya Mifumo ya Ekolojia na Uhifadhi Profesa Pantaleo Munishi amesema msingi wa maisha hapa duniani kwani kila kiumbe hai kinachoonekana ni baianuai

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.