Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Siku 100 kuunda serikali ya umoja Sudani Kusini

Kipindi kipya cha kutokuwa na uhakika na kutawaliwa na hali ya wasiwasi kinafunguliwa kwa nchi ya Sudani Kusini. Kuanzia Jumatano wiki hii Novemba 13, kipindi cha siku 100 kinaanzishwa ili kuwezesha serikali ya umoja inaundwa lakini pia kutafutia suluhu masuala kuhusu usalama na kugawana madaraka.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir akihutubia katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba Novemba 9, 2019.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir akihutubia katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba Novemba 9, 2019. © REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Waliosaini makubaliano ya amani ya mwaka 2018, hususan Rais Salva Kiir na mpinzani wake mkuu Riek Machar, wamekubali kusogezwa mbele kwa mara ya pili mchakato huu wa amani ambao umechelewa sana.

Baada ya kusogezwa mbele kwa mara ya kwanza kwa miezi sita, mchakato huu bado unaonekana kuwa mgumu. maswali mengi yameibuka kuhusu kitakachofanyika na pande husika katika mchakato huo kwa kipindi cha siku 100 na zaidi.

Hivi sasa, Salva Kiir anaandamwa na anakabiliwa na shinikizo kubwa. Jumuiya ya maendeleo ya kikanda (IGAD) imemtaka rais Salva Kiir atoe dola milioni 100 alizoahidi kutekeleza mkataba huo. Upinzani, kwa upande wake, unamshutumu rais Salva Kiir kukataa kufadhili mchakato huo wa amani.

Kwa upande wake Salva Kiir amezitolea wito pande zilizotia saini kwenye mkataba huo kuwa na subira, na kuahidi kwamba atazungumza na pande zote na kwamba pesa zilizobaki zitatolewa.

Lakini, wachunguzi wengi wanakosoa msimamo wa Salva Kiir.

Klem Ryan anabaini kwamba ikiwa kweli Salva Kiir anataka amani, angewaachilia wafungwa wa kisiasa na kufuta sheria yake yenye utata inayoongezea idadi ya majimbo ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa mtafiti huyo, "hatua hizi zinaweza kuchukuliwa wakati wowote, bila mazungumzo ya kweli".

Kwa hivi sasa, pande zote mbili bado ziko kwenye vita vya madaraka, "amebaini mwandishi Mathiang Jalap Dongvin.

Raia kwa upande wao, wanaendelea kusubiri kitakachotokea katika kipindi hiki cha siku 100 na zaidi, lakini hofu inaendelea kutanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.