Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Kiir na Machar wapewa siku 100 kuokoa mchakato wa amani Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, wamepewa siku nyingine 100 ili waunde Serikali ya pamoja baada ya kushindwa kumaliza tofauti zao, uamuzi ambao umekosolewa vikali na Marekani iliyosema taifa hilo linahitaji viongozi wapya.

Salva Kiir na Riek Machar Septemba 12, 2018.
Salva Kiir na Riek Machar Septemba 12, 2018. YONAS TADESSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, "kipindi cha kabla ya mpito", kilichopangwa kuanza tarehe 12 Novemba, kitaongezewa miezi mitatu. Tume ya upatanishi inatarajia kwamba tarehe hii ya mwisho itazuia Sudani Kusini kutumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kulia) akishikana mikono na mpinzani wake Riek Machar, Entebbe, Uganda, Julai 7, 2018.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kulia) akishikana mikono na mpinzani wake Riek Machar, Entebbe, Uganda, Julai 7, 2018. SUMY SADURNI / AFP

Serikali ya mpito ambayo ingezileta pande mbili pamoja ingelikuwa iko tayari mwezi Mei mwaka huu. Lakini, kutokana na kuahirishwa mara ya kwanza, halafu mara ya pili, sasa serikali hiyo inatarajiwa kutangazwa mwezi Februari mwakani. Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamepewa siku 100 kuwapa nafasi ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Maamuzi haya yalifikiwa jijini Kampala, wakati viongozi hawa walipokutana na rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Zoezi la uundaji wa jeshi la umoja linaendelea kuzua mvutano mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.