Pata taarifa kuu
BURUNDI-RSF-VYOMBO VYA HABARI

RSF: Vyombo huru vya habari vyalengwa nchini Burundi

Shirika la Wanahabari Wasiokuwa na Mipaka (RSF) limeinyooshea kidole cha lawama serikali ya Burundi kuwa inalengo la kuwatia uoga waandishi wa habari, hasa wale wa vyombo huru kwa kile shirika hilo limesema wasithubutu kueleza kinaga ubaga yale yanayotokea nchini humo.

Maafisa wa polisi wakiwa katika majengo ya RPA, moja ya redio huru nchini Burundi, Aprili 26, 2015.
Maafisa wa polisi wakiwa katika majengo ya RPA, moja ya redio huru nchini Burundi, Aprili 26, 2015. Photo : RFI / SR
Matangazo ya kibiashara

RSF imeonya kuwa msako wa Burundi unalenga kuvinyamazisha vyombo vyote huru vya habari kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hayo yanajiri wakati wanahabari wanne wa Gazeti la Iwacu na dereva wao wamekuwa wakizuiliwa tangu tarehe 22 Oktoba kwa madai ya kujaribu kuwahoji wakazi wa Bubanza ambao walikuwa wakitoroka mapigano kati ya vikosi vya usalama na waasi.

Wanahabari hao na dereva wao wameshtakiwa kwa madai ya kuhujumu usalama wa taifa, baada ya kuangazia shambulio la waasi katika mji wa Bubanza ulio Kaskazini Magharibi mwa Burundi.

RSF imeonya kuwa msako wa Burundi unalenga kuvinyamazisha vyombo vyote huru vya habari kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
RSF imeonya kuwa msako wa Burundi unalenga kuvinyamazisha vyombo vyote huru vya habari kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. RFI/Sonia Rolley

Oktoba 22, wanahabari wanne wa Gazeti la Iwacu waliotumwa kwenda kuangazia makabiliano kati ya wanajeshi wa nchi hiyo na waasi wa Red Tabara mjini Bubanza walikamatwa na kupokonywa vifaa vyao vya kazi kama vile kamera na simu za rununu.

Walizuiliwa bila kufunguliwa mashataka kwa siku nne kabla ya mwendesha mashtaka wa Bubanza, Clement Ndikuriyo, kutuhumu dereva wao kwa kushirikiana na waasi wa Red Tabara.

Watano hao wameshatakiwa kwa kosa la kukiuka kanuni ya usalama wa kitaifa wa Burundi, kosa ambalo hukumu yake ni kifungo cha miaka 10 jela.

Burundi imeshuhudia msako mkali dhidi ya vyombo vya habari na upinzani tangu mwaka 2015.

vyombo vya habari vya kibinafsi na vile vya kimataifa ikiwemo ikiwa ni pamoja na BBC, VOA vimefungiwa na baadhi ya wanahabari kukimbilia uhamishoni kwa kuhofia usalama wao.

Burundi imeorodheshwa kuwa nchi ya 159 kati ya 180 kwa ukandamizaji wa uhuru wa wanahabari kwa mujibu wa ripoti ya dunia ya RSF ya mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.