Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Hali ya wasiwasi yaendelea kutanda Sudani Kusini

Mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini yameahirishwa kwa siku mbili, wakati huu kukiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya umoja ifikapo Novemba 12.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kulia) na mpinzani wake Riek Machar wakisabahiana kwa kupeana mikono. Julai 7, 2018.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kulia) na mpinzani wake Riek Machar wakisabahiana kwa kupeana mikono. Julai 7, 2018. SUMY SADURNI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya rais Salva Kiir na mwenzake Riek Machar yalikuwa yafanyike Jumanne wiki hii lakini yakaahirishwa bila ya uwepo wa sababu za msingi.

Taarifa kutoka taasisi zinazosimamia mchakato wa amani nchini humo, zinasema kuwa viongozi hao wawili hawajaonesha nia ya kuwa tayari kufanya kazi pamoja.

Aidha madai ya rais Kiir kuwa ataunda Serikali peke yake bila ya Machar yanazidisha sintofahamu zaidi kuhusu mustakabali wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.